Serikali ya Kenya imetangaza kuwa itaanza kufungua hoteli zake kwa kuzingatia masharti ya kuwapima wahudumu wa afya na ikiwa hawatakuwa na maambukizi ya virusi vya Corona ndio wataweza kuhudumu kwenye hoteli hizo.
Taarifa hii ya hoteli kuanza kufunguliwa imetangazwa na Waziri wa Afya nchini humo Mutahi Kagwe ambapo amesema kuwa hoteli hizo zitahitajika kufuata kanuni zitakazowekwa kama vile kuhakikisha kuwa hakuna misongamano katika hoteli hizo.
Idadi ya watu waliopona virusi vya Corona imetajwa kuongozeka nchini humo na kufikia 114 baada ya watu 8 hii leo kuruhusiwa kutoka hospitalini.
Aidha, Waziri Kagwe amesema pia wagonjwa wameongezeka na kufikia 363 kwa ongezeko la watu 8 waliokutwa na maambukizi kuongezeka leo baada ya kupimwa na kukutwa na maambukizi ya Virusi vya Corona.
Wagonjwa hao 8 walioripotiwa leo wote wametolewa ufafanuzi kuwa ni raia wa Kenya na wala hakuna wa nje ya nchi hiyo.