Star Tv

Wanafunzi wawili wa Shule ya sekondari ya Wasichana ya Buruburu nchini Kenya wamefikishwa mahakamani leo Jumatatu kuhusiana na kisa cha moto katika shule hiyo kilichotokea wiki iliyopita na kusababisha wanafunzi 59 kulazwa hospitalini.

Wawili hao wanadaiwa kupanga na kuchoma moja ya bweni mnamo Oktoba 31 kabla ya kutoroka na kuwaacha wenzao wakiwa ndani, Citizen Digital imeripoti.

Wakati huo huo, Waziri wa Elimu George Magoha ameonya kwamba wanafunzi wote wanaohusika katika tukio la uchomaji shule watakabiliwa na mkono wa sheria.

Kikao kati ya Bodi ya Menejimenti na Jumuiya ya Wazazi na walimu kiliazimia mambo kadhaa ambayo ni pamoja na uwekaji wa kamera za CCTV shuleni hapo, milango ya kutokea ya dharura iliyofunguliwa moja kwa moja kwenda nje ili ifanye kazi na kukaguliwa mara kwa mara ili kuimarisha ulinzi na usalama shuleni hapo.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.