Bodi ya Filamu Kenya inasema kuwa filamu kuhusu maisha ya wanandoa wa jinsia nchini Kenya imepigwa marufuku nchini humo.
Katika taarifa KFCB imesema filamu ya I am Samuel, inahamasisha ndoa ya wapenzi wa jinsia moja ambayo inakiuka sheria inayoharamisha ushoga.
Iliongeza kuwa filamu hiyo pia ilikuwa "inabeza katiba inayotambua familia kama msingi wa jamii na inafafanua ndoa kuwa kati ya watu wawili wa jinsia tofauti".
"Jaribio la kufanya onyesho, kusambaza, kutangaza au kuwa na filamu hiyo iliyopigwa marufuku nchini Kenya kutakabiliwa kisheria,”- Chris Wambua, Kaimu Mkuu wa Bodi ya Filamu, aliwaambia wanahabari.
Filamu hiyo, iliyoelekezwa na Peter Murimi, ilitolewa mwaka jana, ni filamu iliyoandaliwa kwa zaidi ya miaka mitano na inaangazia uhusiano wa Sam na mpenzi wake Alex dhidi ya kuongezeka kwa vurugu na ubaguzi.
Aidha, KFCB ilitoa uamuzi juu ya filamu hiyo kwani ilikuwa imeombwa kuipa uainishaji.
#ChanzoBBCSwahili