Star Tv

Naibu wa Rais nchini Kenya William Ruto amemjibu waziri wa msuala ya ndani nchini Kenya Fred Matiangi kufuatia matamshi yake mbele ya kamati moja ya bunge siku ya Jumatano.

Kulingana na taarifa ilitolewa na msemaji wake David Mugonyi, na kunukuliwa na gazeti la The People Daily nchini Kenya, naibu huyo amemkosoa waziri Matiangi kwa kutoa matamshi yasio na msingi.

Kulingana na naibu huyo lengo la Matiangi katika kikao hicho cha kamati ya bunge lilikuwa kumdhalilisha na kumkejeli yeye na afisi yake.

"Kulingana na matamshi yaliotolewa na waziri Matiangi hakuna ushahidi kwamba anataka kuelewa katiba ama hata wasiwasi uliopo kuhusu usalama wa naibu wa rais’’-alisema Mugonyi.

Aidha, taarifa yake iliendelea kufafanua kuwa "Bwana Matiangi ametumia vibaya rasilimali ya umma na uwezo wa ofisi yake kwa maslahi ya kisiasa ili kumdhalilisha na kuikejeli ofisi ya William Ruto kwa propaganda za kisiasa’’.

Kulingana na Gazeti la The People, amemshtumu Matiangi na kusema hatua yake inahatarisha usalama wa maisha ya naibu wa rais William Ruto.

Latest News

UFARANSA YAZINDUA MAGARI YA UMEME HAPA NCHINI.
20 Oct 2021 15:31 - Grace Melleor

Waziri wa Biashara na uchumi nchini Ufaransa Franck Riester amezindua magari ya umeme yaliyoundwa na kampuni ya E-Motion [ ... ]

UHITAJI WA NYAMA WAONGEZEKA NCHINI.
20 Oct 2021 15:23 - Grace Melleor

Serikali imesema malalamiko yaliyojitokeza hivi karibuni ya kupanda kwa bei ya nyama nchini yanaashiria ukuaji wa sekta  [ ... ]

UGANDA YAZINDUA GARI LA KIVITA LILILOUNDWA NCHINI HUMO.
19 Oct 2021 18:03 - Grace Melleor

Jeshi la Uganda limezindua gari la kivita lililoundwa nchini humo.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.