Star Tv

Rais wa Uganda Yoweri Museveni, leo anaanza safari ya kutoka kijijini kwao akielekea mji wa Kampala ambapo atakuwa anasimama katika vituo kadhaa kwenye miji mbalimbali kutoa shukrani kwa wananchi.

Rais Museveni aliyeshinda tena uchaguzi wa urais wiki iliyopita ili kuongoza kwa muhula wa sita atasimama katika vituo saba akiwa njiani kurejea Kampala.

Msemaji wa serikali Ofwono Opondo ameandika taarifa za kina juu ya safari hiyo kwenye mtandao wa Twitter.

Safari hiyo ya Rais inawadia wakati wito umetolewa kwa serikali kuondoa kifungo cha nyumbani dhidi ya kiongozi wa upinzani Robert Kyagulanyi, maarufu kama Bobi Wine, ambaye anapinga matokeo ya uchaguzi.

Marekani imetoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi katika madai ya wizi wa uchaguzi yaliyoibuliwa na upande wa upinzani ambao bado haujafanikiwa kuwasilisha ombi rasmi la kupinga matokeo.

Ofisi za upinzani zilivamiwa na jeshi na maafisa wa chama hicho wanasema nyenzo walizokuwa wanazikusanya kwa ajili ya kupinga matokeo ya uchaguzi walinyang’anywa na maafisa hao.

Latest News

SHAMBULIO LA KUJITOA MHANGA LAUA WATU NANE SOMALIA.
25 Nov 2021 10:26 - Grace Melleor

Polisi nchini Somalia wamethibitisha vifo vya raia katika bomu lililotegwa ndani ya gari katika mji mkuu Mogadishu, tele [ ... ]

WAZIRI MKUU SWEDEN AJIUZULU SAA CHACHE BAADA YA KUTEULIWA.
25 Nov 2021 09:01 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke kuwahi kushikilia wadhifa huo nchini Sweden amejiuzulu saa chache mara baada ya kuteuliwa [ ... ]

MTOTO WA GADDAFI AZUIWA KUGOMBEA URAIS LIBYA.
25 Nov 2021 07:13 - Grace Melleor

Mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa Libya hayati Muammar Gaddafi ameenguliwa katika kinyang’anyiro cha kuwania uchaguzi wa  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.