Star Tv

Serikali ya Somalia imekatisha uhusiano wa kidiplomasia na nchi ya Kenya.

Nchi hiyo imewaita nyumbani wanadiplomasia wake wote kutoka Nairobi na kuwapatia wanadiplomasia wa Kenya muda wa siku 7 kuondoka nchini humo.

Tangazo hilo limetolewa na Waziri wa Habari Osman Abukar Dubbe katika chombo cha habari cha kitaifa.

"Serikali ya Somali, kulingana uhuru wake iliyohakikishiwa na sheria ya kimataifa, inatekeleza wajibu kwa mujibu wa katiba ili kulinda utaifa, umoja na ustawi wa nchi imeamua kukatiza uhusiano wake wa kidiplomasia na serikali ya Kenya"- alisema.

Hatua hiyo inakuja baada ya Somalia kuwasilisha barua ya malalamiko dhidi ya Kenya kwa Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Viongozi wa nchi wanachama wa muungano wa maendeleo Afrika Mashariki na pembe ya Afrika (IGAD).

Hivi karibuni Somalia iliituhumu Kenya kwa kuingilia masuala yao ndani.

Latest News

SHAMBULIO LA KUJITOA MHANGA LAUA WATU NANE SOMALIA.
25 Nov 2021 10:26 - Grace Melleor

Polisi nchini Somalia wamethibitisha vifo vya raia katika bomu lililotegwa ndani ya gari katika mji mkuu Mogadishu, tele [ ... ]

WAZIRI MKUU SWEDEN AJIUZULU SAA CHACHE BAADA YA KUTEULIWA.
25 Nov 2021 09:01 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke kuwahi kushikilia wadhifa huo nchini Sweden amejiuzulu saa chache mara baada ya kuteuliwa [ ... ]

MTOTO WA GADDAFI AZUIWA KUGOMBEA URAIS LIBYA.
25 Nov 2021 07:13 - Grace Melleor

Mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa Libya hayati Muammar Gaddafi ameenguliwa katika kinyang’anyiro cha kuwania uchaguzi wa  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.