Jeshi la Kenya Defence Forces (KDF) limendelea kuwa na umaarufu wake katika Bara la Afrika kutokana na mafunzo na ushirikiano na nchi kama Israel, Marekani na Uingereza.
Hatua hii ya KDF kudhihirika kuwa ni maarufu barani Afrika inakuja wakati jeshi lilipoadhimisha kumbukizi ya siku yake hapo jana Octoba 14, inayojulikana kama KDF Day.
Hata hivyo tishio kubwa linaloendelea kuyakabili majeshi ya ukanda huu ni kundi la kigaidi la Al shabab ambalo limesababisha maelfu ya watu kupoteza maisha na wengine kulazimika kutoroka jeshini.
Jeshi la Kenya linaendelea kukabiliana na mashambulizi mbalimbali nchini Somalia na Kenya.
Tarehe 14 Oktoba ni siku ya wanajeshi wa Kenya maarufu kama 'KDF day', Ambapo rais Uhuru Kenyatta alihudhuria sherehe hizo katika kambi ya kijeshi ya Lanet huko Nakuru.
Rais Kenyatta alitumia fursa hiyo kuwakumbuka wanajeshi waliofariki dunia katika vita dhidi ya kundi la Al Shabab nchini Somalia, huku Wanajeshi wa Kenya na jamaa zao wakishiriki kwa amani sherehe hizo maalum kuadhimisha siku hiyo ya idara ya jeshi la Kenya KDF.