Star Tv

Rwanda imehalalisha kisheria ukulima na mauzo ya nje ya nchi ya mmea wa bangi kwa ajili ya matumizi ya tiba ili kupata fedha.

Kupitia Kikao cha baraza la mawaziri kilichokaa Jumatatu kiliidhinisha “miongozo juu ya ukulima, usindikaji na mauzo ya nje ya mimea ya matibabu ya thamani ya juu nchini Rwanda ”.

Akizungumza na televisheni ya taifa hilo Waziri wa afya wa Rwanda Dkt. Daniel Ngamije alisema mimea hiyo inajumuisha bangi.

Taifa hilo lililopo ndani ya Bara la Afrika Mashariki limehalalisha bangi baada ya nchi kama Malawi, Lesotho, Afrika Kusini, Zambia na Zimbabwe kuhalalisha kisheria mauzo ya bangiau matumizi ya mmea huo.

Bwana Ngamije amesema "Rwanda inataka kutoa mchango wake kwa vituo vya utafiti na sekta ya madawa kwa kutoa raslimali ili tupate faida ya fedha…”

Kulingana na Benki ya Bardays imebainisha kuwa Mwaka jana, soko la bangi la dunia lilidhaniwa kuwa na thamani ya dola bilioni 150.

Aidha, kufuatia hatua hiyo ya Rwanda kwa mmea wa bangi mpaka sasa ruhusa ni kwa wakulima pekee ndio waliopewa leseni, ambao wataruhusiwa kuzalisha zao hilo huku uvutaji wa bangi bado unazuiwa.

Bodi ya maendeleo ya Rwanda imesematoa angalizo kwa wananchi wa Rwanda kuwa iwapo utapatikana unalima au kuuza bangi nchini bila kibali kutoka mamlaka husika unaweza kuadhibiwa hadi kifungo cha maisha jela , huku mvutaji akikabiliwa na kifungo cha miaka miwili jela nchini Rwanda.

 

Latest News

BIDEN KUSAINI MAAGIZO 12 YA RAIS.
17 Jan 2021 07:08 - Grace Melleor

Rais mteule wa Marekani Joe Biden atatia saini maagizo 12 ya rais siku ya kuapishwa kwake kuwa rais wiki ijayo ili kushu [ ... ]

MUSEVENI AWAONYA WAFUASI WA UPINZANI KUTOZUA GHASIA.
17 Jan 2021 06:10 - Grace Melleor

Rais wa muda mrefu nchini Uganda Yoweri Museveni jana Jumamosi ameonya kuwa vikosi vya usalama vitatumia nguvu kuzima ju [ ... ]

WATU WAWILI WANUSURIKA KUAWA NA WANANCHI WENYE HASIRA KALI.
17 Jan 2021 05:42 - Grace Melleor

Watu wawili wakazi wa Manispaa ya Musoma mkoani Mara wamenusurika kuawa na wananchi wenye hasira kali kutoka kwa vijana  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.