Star Tv

Mahakama ya katiba nchini Angola imetupilia mbali madai ya chama cha upinzani UNITA kuyafuta matokeo ya uchaguzi yaliyokipa ushindi chama tawala cha MPLA.

UNITA ilipeleka malalamiko yake mahakamani baada ya tume ya uchaguzi wiki iliyopita kumtangaza rais Joao Lourenco kushinda muhula wa pili madarakani, ikitoa hija kwamba tume hiyo haiku-kishirikisha ipasavyo katika hatua za mwisho za kuidhinisha matokeo. Hata hivyo mahakama ya katiba Angola imesema chama cha UNITA kinachoongozwa na Adalberto Costa Junior hakikukidhi matakwa yaliyohitajika ili kuwezesha matokeo hayo kufutwa. Matokeo ya tume ya uchaguzi yaliyotangazwa wiki iliyopita yalikipa ushindi chama cha MPLA kwa asilimia 51.17 ya kura na UNITA ikapata asilimia 43.9 ya kura.

CHANZO: DW SWAHILI

Latest News

MUHUDUMU MWINGINE AFARIKI KWA EBOLA UGANDA.
05 Oct 2022 12:44 - Grace Melleor

Wizara ya afya nchini Uganda imethibitisha kifo cha mhudumu mwingine wa afya, ambaye amefariki alfajiri ya leo Jumatano. [ ... ]

KIONGOZI MKUU WA IRAN AILAUMU MAREKANI NA ISRAEL.
04 Oct 2022 14:14 - Grace Melleor

Kiongozi mkuu wa Iran amezilaumu Marekani na Israel kwa kuchochea maandamano yaliyoenea nchini humo kufuatia kifo cha mw [ ... ]

WAHITIMU 1,384,340 KUANZA MTIHANI.
04 Oct 2022 13:56 - Grace Melleor

Jumla ya watahiniwa 1,384,340 wanatarajia kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi utakaofanyika Oktoba tano na sita  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.