Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imefungua awamu ya pili ya maombi ya udahili wa shahada ya kwanza kwa mwaka wa masomo 2022/2023.
Hayo yamebainishwa leo Agosti 24, 2022 na Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Charles Kihampa amesema idadi hiyo ni sawa na asilimia 70.72 ya waombaji wote ambao walituma maombi katika awamu ya kwanza ya udahili.
Awamu hiyo ya pili ya udahili itafungwa Septemba 6, 2022 na
kufunguliwa kwa dirisha hilo kunakwenda sambamba na kufungwa kwa awamu ya kwanza ya udahili inayoonyesha waombaji 75,163 wamepata nafasi.