Mkazi mmoja Wilayani Serengeti aitwaye Happy Nyasumo mwenye umri wa miaka 18 amemuua mumewe, Bebe Mbogo (26) kwa madai kuwa hampendi na hakuwa chaguo lake zikiwa zimepita siku 14 tangu walipofunga ndoa yao.
Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Nurdin Babu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema mwanamke aliyefanya kitendo hicho dhidi ya mumewe amekiri kweli kumuua mumewe.
Aidha, Happy amedai kuwa kabla ya yeye kutekeleza mauaji hayo mumewe alimlazimisha kufanya tendo la ndoa na baada ya kumaliza mwanaume alilala na yeye alipobaini amesinzia akachukua panga na kumkata mara tatu shingoni kwasababu hafikirii kama mumewe alikuwa chaguo lake kwa vitendo alivyokuwa akimfanyia.
Aidha mtuhumiwa tayari ameshafikishwa kituo cha polisi ili kuchukuliwa hatua zaidi