Kiongozi wa Upinzani nchini Kenya Raila Odinga, amesema hali yake ni nzuri na anafuata ushauri wa madaktari kwa kupumzika.
Odinga alifanyiwa uchunguzi wa kawaida wa kimatibabu katika hospitali ya Nairobi siku ya Jumanne hatua iliyozua hofu kuhusu hali yake ya afya.
Madaktari wake wakiongozwa na daktari wake wa kibinafsi, Dkt. David Olunya, walisema Waziri Mkuu huyo wa zamani alikuwa ameshauriwa kupumzika baada ya kuhisi amechoka.
"Raila alienda kufanyiwa uchunguzi wa kawaida wa matibabu katika Hospitali ya Nairobi mnamo Machi 9 baada ya kuhisi uchovu. Amekuwa na kampeni kali na alihitaji kufanyiwa uchunguzi. Hii ilifanyika kwa mafanikio"-Amesema Mtaalamu wa Upasuaji wa Neva Dkt. Olunya, .
Odinga baadaye alitumia mtandao wake wa kijamii wa twitter kuwashukuru wote waliomtakia afueni ya haraka na akiwahakikishia kwamba hali yake ni nzuri.
Chanzo: BBC Swahili.