Star Tv

Picha mbalimbali za matukio ya msiba wa aliyekuwa Makamu wa kwanza wa rais Zanzibar baada ya kuwasili katika viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo maelfu wamejitokeza kuomboleza msiba huo uliotokea jana Februari 17,2021.

Viongozi mbalimbali ikiwemo marais wastaafu wa Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Shein, Abeid Amani Karume na wengine wamehudhuria mazishi ya Maalim Seif Sharif Hamad

Kisiwani Pemba ambapo ndio ilikuwa ngome yake Kuu wakati wa uhai wake, punde tu baada ya taarifa za kifo chake kuenea hapo jana, baadhi ya maduka yamefungwa na shughuli nyingi za mji kusimama, hivyo kufanya mji huo kuzizima kwa saa kadhaa.

Ratiba ya mazishi inaonyesha kuwa, mwili wa marehemu utakwenda kupumzishwa kijijini kwao Mtambwe-Pemba.

#RIPMaalimSeifSharifHamad

Latest News

RAIS MAGUFULI AWAONYA WAKANDARASI WANAOCHELEWESHA MIRADI.
24 Feb 2021 13:33 - Grace Melleor

Rais John Magufuli amezindua barabara ya juu eneo la Ubungo ambayo imepewa jina la Marehemu John Kijazi, ambaye alikuwa  [ ... ]

MWILI WA BALOZI WA ITALIA WASAFIRISHWA KWENDA ROMA.
24 Feb 2021 09:52 - Grace Melleor

Mwili wa balozi wa Italia aliyeuawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika jaribio la utekaji nyara uliotibuka s [ ... ]

MWANASIASA WA UPINZANI WA RWANDA AUAWA.
22 Feb 2021 07:59 - Grace Melleor

Mwanasiasa wa upinzani na raia wa Rwanda anayeishi mafichoni nchini Afrika Kusini ameuawa kwa kupigwa risasi.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.