Star Tv

Wanajeshi wanne wa Mali wameuawa katika shambulio lililotokea katikati mwa nchi hiyo Jumarano wiki hii.

Taarifa kutoka vyanzo vya usalama vinaeleza kuwa Wanajeshi hao waliuawa katikati mwa Mali, moja ya maeneo makuu yanayokabiliwa na machafuko mabaya tangu miaka kadhaa nchi hiyo ikiwa katika vita, kulingana na vyanzo vya usalama.

Shirika la habari la AFP limenukuu taarifa kutoka Wizara ya Usalama na serikali ya eneo hilo ambayo imebainisha kuwa Shambulio hilo lilitokea karibu na mji wa Alatona, ambapo si mbali na mji wa Niono,

Wakati huo huo Imam Mahmoud Dicko, kiongozi wa kidini mwenye ushawishi mkubwa nchini Mali ametoa wito kwa viongozi wa jeshi kutekeleza amri ya viongozi wa jumuiya ya Afrika Magharibi ya kumteua Rais na Waziri Mkuu kufikia septemba 15 ili kulegeza vikwazo vilivyowekwa mwezi uliopita.

Hapo jana, Dicko ameliambia shirika la taifa la habari kwamba nchi hiyo inahitaji usaidizi na kwamba haifaidiki na chochote kwa kwenda kinyume na jamuiya kimataifa.

Chanzo:rfi Swahili.

Latest News

JAJI MKUU WA KENYA AMSIHI RAIS KENYATTA KULIVUNJA BUNGE.
22 Sep 2020 10:22 - Grace Melleor

Jaji Mkuu wa Kenya David Maraga, amemshauri rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta, kulivunja bunge la kitaifa na lile la Sene [ ... ]

“IRAN ITAJIBU VIKALI UONEVU WA MAREKANI"- Rais Hassan Rouhani.
21 Sep 2020 11:51 - Grace Melleor

Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema Marekani imeshindwa katika juhudi zake za kuiwekea tena vikwazo nchi hiyo baada ya w [ ... ]

UGANDA YAENDELEA KULEGEZA VIZUIZI DHIDI YA CORONA.
21 Sep 2020 06:31 - Grace Melleor

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza kuwa shule na taasisi zingine za elimu ya juu, zitafunguliwa tena kuanzia mwez [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.