Star Tv

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, na mkewe, Maria, wamepata watoto wengine wawili mapacha ambao ni Mapacha wa kiume na wa kike.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Makonda amethibitisha kuwa mkewe Maria amejifungua na kufanya idadi ya watoto wao kufikia watatu sasa na kuandika ujumbe wa kumshukuru Mungu kwa zawadi hiyo ya Watoto wawili.

"Heshima na Mamlaka ni zako eee Mungu wa Mbingu na Nchi na kwako wewe tunalia Aba, nitaendelea kutaja ukuu wako siku zote za maisha yangu kwakuwa hujawahi kuniacha hata dakika moja"-Ameandika Makonda.

Makonda aliendeleza ujumbe wa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuendelea kuandika;
"Pamoja na mapito magumu na mazito lakini naiona nuru yako huku nikisikia sauti ya ROHO mtakatifu ikisema mwanangu Paul Christian Makonda nalikujua kabla sijakuumba na nikakutenga kwa kusudi langu usikubali TAA iwakayo ndani yako ikazimika, Ona sasa unavyozidi kuniheshimisha katikati ya machozi umenipatia zawadi tena itokayo kwako".

"Mimi nilieitwa tasa ulinipa mtoto KEAGAN ambaye alishangaza ulimwengu kwa ujio wake: Ukaona haitoshi LEO umenipa DOUBLE PORTION:Leo Mungu wangu umenipa MAPACHA tena wa KIUME na Wa KIKE hii yote ni kutangaza UKUU wako maishani mwangu"-Makonda.

"Kwa wale ambao bado hawajakuamini na wanateseka juu ya uzazi,naomba kupitia watoto hawa wakauone ukuu wako Ewe YESU mwana wa Mungu ulie hai. Hongera sana kipenzi changu Maria Mungu amejitwalia utukufu kupitia wewe"-Anaendelea kuandika Makonda.

"Asanteni sana watumishi wa Mungu, wazazi wetu, dada na kaka zetu kwa kuwa nasi nyakati zote, kama ambavyo mmekuwa baraka kwetu.Naomba pia Mungu awainulie watu wema nyakati za uhitaji wenu"-Makonda.

Aidha, Makonda alihitimisha ujumbe wake wa kutoa shukrani kwa Mungu kwa kuweka hashtag iliyoambatana na maneno haya;#EhhNafsiYanguMUHIMIDI-Bwana, #MoyoWaShukrani.

Latest News

JAJI MKUU WA KENYA AMSIHI RAIS KENYATTA KULIVUNJA BUNGE.
22 Sep 2020 10:22 - Grace Melleor

Jaji Mkuu wa Kenya David Maraga, amemshauri rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta, kulivunja bunge la kitaifa na lile la Sene [ ... ]

“IRAN ITAJIBU VIKALI UONEVU WA MAREKANI"- Rais Hassan Rouhani.
21 Sep 2020 11:51 - Grace Melleor

Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema Marekani imeshindwa katika juhudi zake za kuiwekea tena vikwazo nchi hiyo baada ya w [ ... ]

UGANDA YAENDELEA KULEGEZA VIZUIZI DHIDI YA CORONA.
21 Sep 2020 06:31 - Grace Melleor

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza kuwa shule na taasisi zingine za elimu ya juu, zitafunguliwa tena kuanzia mwez [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.