Star Tv


Mafuriko yaliyotokea wiki hii nchini Afghanistan yamegharimu maisha ya karibu watu 160 na waokoaji wanaendelea kutafuta watu ambao wamekwama kwenye matope na chini ya vifusi vya nyumba zilizosombwa na maji, mamlaka imesema.

Mikoa kumi na tatu, hasa kaskazini mwa nchi, imeathirika, kulingana na wizara yenye dhamana ya kukabiliana na majanga.

Katika mkoa wa Parwan peke yake, kaskazini mwa Kabul, watu 116 wamepoteza maisha, zaidi ya 120 wamejeruhiwa na 15 bado hawajulikani waliko, viongozi wamesema.

Wizara ya ulinzi imebaini kwamba vikosi vya usalama vya Afghanistan vimekuwa vinasaidia katika shughuli ya uokoaji na kutoa misaada, licha ya kukabiliwa na ghasia zinazotekelezwa na Taliban nchini humo.

Wizara ya ulinzi imebaini kwamba vikosi vya usalama vya Afghanistan vimekuwa vinasaidia katika shughuli ya uokoaji na kutoa misaada, licha ya kukabiliwa na ghasia zinazotekelezwa na Taliban nchini humo.

Jumuiya ya kujihami ya nchi za Magharibi, NATO, imesema vikosi vyake vikilisaidia jeshi la Afghanistan vimepeleka chakula, maji na blanketi kwa maeneo yaliyoathiriwa.

 

Latest News

JAJI MKUU WA KENYA AMSIHI RAIS KENYATTA KULIVUNJA BUNGE.
22 Sep 2020 10:22 - Grace Melleor

Jaji Mkuu wa Kenya David Maraga, amemshauri rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta, kulivunja bunge la kitaifa na lile la Sene [ ... ]

“IRAN ITAJIBU VIKALI UONEVU WA MAREKANI"- Rais Hassan Rouhani.
21 Sep 2020 11:51 - Grace Melleor

Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema Marekani imeshindwa katika juhudi zake za kuiwekea tena vikwazo nchi hiyo baada ya w [ ... ]

UGANDA YAENDELEA KULEGEZA VIZUIZI DHIDI YA CORONA.
21 Sep 2020 06:31 - Grace Melleor

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza kuwa shule na taasisi zingine za elimu ya juu, zitafunguliwa tena kuanzia mwez [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.