Star Tv

Mkutano wa pili wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, unafanyika leo Ijumaa Agosti 28082020 tangu kufanyika kwa mapinduzi nchini Mali.

Tangu wiki iliyopita kundi la jeshi linaloshikilia madaraka limeendelea kupata shinikizo ili kurejesha taasisi za kiraia zilizochaguliwa.

Wiki iliyopita Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS ililita jeshi kumrejesha madarakani Ibrahim Boubacara Keita, na kuchukua uamuzi wa kufunga mipaka ya nchi wanachama jirani na Mali na kuiwekea nchi hiyo vikwazo vya kiuchumi. Lakini tangu wakati huo jeshi lilianza kulegeza msimamo wake. Jeshi lilikubali kumuachilia huru rais aliyepinduliwa Ibrahim Boubacar Keita.

Wakati huo huo mazungumzo kati ya wanajeshi wanaoshikilia madaraka nchini Mali na ECOWAS kuhusu uundwaji wa serikali ya mpitoa yameanza. Jumuiya hiyo imelitaka jeshi kuunda serikali ya mpito itakayoongoza nchi kwa mwaka mmoja.

ECOWAS "inakubali" wazo la "serikali ya mpito itakayoyoongozwa na raia au mwanajeshi mstaafu" kwa kipindi cha mpito cha "miezi sita, tisa, au kumi na mbili" nchini Mali, kabla ya kufanyika kwa uchaguzi nchini humo, imesema taarifa kutoka ikulu ya rais wa Nigeria.

Taarifa hiyo ikimaanisha kuwa miezi hiyo waliyoitaja ni sawa na kipindi cha mwaka mmoja, huku jeshi la Mali likiwa linataka "kukaa madarakani" kwa "miaka mitatu" kabla ya kufanyika uchaguzi.

Latest News

JAJI MKUU WA KENYA AMSIHI RAIS KENYATTA KULIVUNJA BUNGE.
22 Sep 2020 10:22 - Grace Melleor

Jaji Mkuu wa Kenya David Maraga, amemshauri rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta, kulivunja bunge la kitaifa na lile la Sene [ ... ]

“IRAN ITAJIBU VIKALI UONEVU WA MAREKANI"- Rais Hassan Rouhani.
21 Sep 2020 11:51 - Grace Melleor

Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema Marekani imeshindwa katika juhudi zake za kuiwekea tena vikwazo nchi hiyo baada ya w [ ... ]

UGANDA YAENDELEA KULEGEZA VIZUIZI DHIDI YA CORONA.
21 Sep 2020 06:31 - Grace Melleor

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza kuwa shule na taasisi zingine za elimu ya juu, zitafunguliwa tena kuanzia mwez [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.