Star Tv

Rais wa Marekani mara kadhaa amesikika akisema atalituma jeshi kukabiliana na waandamanaji katika miji mbalimbali nchini Marekani.

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kutumwa kwa vikosi vya usalama katika miji ambayo hivi karibuni imeshuhudia machafuko wakati wa maandamano ya kulaani vitendo vya ubaguzi wa rangi nchini humo.

Miji mingi itakayoshuhudia kupelekwa kwa maafisa wa usalama inaongozwa na chama cha Democratic kama Chicago, New York, Philadelphia na Minneapolis.

Trump amesema hana budi kutuma maafisa hao wa usalama kuwalinda raia.

Hatua hii hata hivyo, imelaaniwa vikali na wanasiasa wa chama cha Democartic kwa kile alichosema, rais Trump anachukua uamuzi huo kupata umaarufu wa kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu mwezi Novemba.

Trump amewashtumu Mameya wa miji inayoongozwa na chama cha Democratic kwa kuwaogopa waandamanaji anaowashtumu kufuja na kuharibu mali ya watu kwa sababu za kisiasa.

Mji wa Portland umekuwa ukishuhudia maandamano dhidi ya ukatili unaotekelezwa na polisi mjini humo tangu kutokea kwa mauaji ya George Floyd, Mmarekani mweusi aliyeuawa akiwa mikononi mwa polisi huko Minnesota mnamo mwezi Mei mwaka huu.

Maafisa 150 wanatarajiwa kutumwa Chicago wiki hii, ili kusaidia maafisa wengine wa serikali pamoja na maafisa polisi wa Chicago kupambana na uhalifu.

Latest News

TEMBO 170 KUPIGWA MNADA NAMIBIA.
03 Dec 2020 10:05 - Grace Melleor

Tembo 170 watapigwa mnada nchini Namibia kwa kile kilichobainishwa kuwa ni adha ya kuongezeka kwa ukame huku kukishuhudi [ ... ]

BOKO HARAM WAKIRI KUTEKELEZA MAUAJI YA WAKULIMA 78.
02 Dec 2020 08:42 - Grace Melleor

Wanamgambo wa kundi la Kiislamu la Boko Haram wametoa video mpya ambayo inasema wapiganaji wake wa Boko Haram ndio walio [ ... ]

BOBI WINE AAHIRISHA KAMPENI ZA URAIS.
02 Dec 2020 08:19 - Grace Melleor

Mgombea wa urais nchini Uganda Robert Kyagulanyi, anayefahamika zaidi kama Bobi Wine ameahirisha kampeni zake.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.