Star Tv

Rais Magufuli ameagiza kusimamishwa kazi kwa Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Arumeru na Afisa Usalama wa Wilaya hiyo mkoani Arusha kwa kushindwa kutimiza majukumu yao.

Akizungumza wakati wa kuwaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni, Rais Magufuli amesema kuwa viongozi hao wameshindwa kutimiza wajibu wao wa kukabiliana na dawa za kulevya, hadi maofisa kutoka makao makuu walipofika na kubaini uwepo wa kiwango kikubwa cha bangi.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amempandisha cheo James Kaji kuwa Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ambapo awali alikuwa akikaimu nafasi hiyo.

Akitangaza uamuzi huo wa kumthibitisha Kaji pamoja na kumuapisha, Rais Magufuli amesema anachotaka kuona ni matokeo ya kazi wanazofanya wasaidizi wake  na kuacha uzembe kwa kile alichokitaja kuwa kunakuwepo na matatizo sehemu mbalimbali nchini lakini wapo baadhi.

 

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.