Star Tv

Baraza la mji wa Minneapolis laahidi kuvunja idara ya polisi kufuatia kifo cha George Floyd, Ambapo idadi kubwa ya maafisa wa baraza la mji huo wameiona hatua hiyo kama ni ya muhimu huku kukiwa na maandamano ya kitaifa yanayoendelea kutokana na kifo cha Mmarekani huyo mweusi kilichotokea mwezi uliopita.

Madiwani tisa kati ya 13 walisema kwamba mfumo mpya wa kuweka usalama wa umma utabuniwa katika mji ambao wasimamizi wa usalama wameshutumiwa kuwa ubaguzi.

Hatahivyo mikakati ya kiusalama kote nchini humo iliondolewa siku ya Jumapili huku hali ya wasiwasi ikiendelea kupungua.

Maandamano hayo yalianza baada ya kanda ya video kuonekana ikimuonyesha Floyd amelazwa barabarani, huku afisa wa polisi mzungu akiwa amemuwekea goti shingoni kwa takribani dakika tisa, huku afisa wa polisi Derek Chauvin amefutwa kazi na kushtakiwa kwa kutekeleza mauaji ya mtu huyo.

Maafisa wengine watatu ambao walikuwa katika eneo hilo pia wamefutwa kazi na kushtakiwa kwa kuruhusu na kuendeleza kilichotokea.

Madiwani tisa walisoma taarifa kwa mamia ya waandamanaji siku ya Jumapili.

''Tuko hapa kwasababu hapa Minneapolis na miji mingine kote Marekani ni wazi kwamba mfumo uliopo wa usalama haulindi jamii'', alisema rais wa baraza hilo Lisa Bender ambaye alinukuliwa akisema pia ''Juhudi zetu za kufanya mabadiliko zimefeli moja kwa moja''.

Bi Bender alisema kwamba maelezo kuhusu uvunjaji huo yanahitajika kujadiliwa zaidi, akiongezea kwamba atajaribu kuhamisha ufadhili wa polisi kwa mikakati inayowekwa na jamii.

Mbadiliko hayo katika baraza la Minneapolisi pia yanaweka kile kinachotarajiwa kuwa mjadala mrefu na mgumu kuhusu njia mpya ya kuweka usalama nchini Marekani.

Meya wa mji wa York City Bill de Blasio alikuwa tayari amesema atahamisha fedha kutoka katika idara ya polisi hadi katika huduma za kijamii.

Aidha, Baraza hilo pia linaonelea kuwa kuondoa ufadhili wa kifedha katika idara ya polisi ni wito uliotolewa katika maandamano ya hivi karibuni ambayo yalibadilika na kukumbwa na ghasia.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.