Star Tv

Kifo cha mhamiaji aliyeshambuliwa mchana kweupe nchini Italia kimezua hasira.

Shambulio dhidi ya mfanyabiashara huyo raia wa Nigeria lililotekelezwa mtaani na mwanamume mwingine katika kituo cha mji wa Civitanova Marche lilinaswa kwenye video siku ya Ijumaa.

Video hiyo, iliyochukuliwa na watazamaji bila jaribio lolote la kuingilia kati, inaonyesha mwathirika akiwa ameshikiliwa chini na raia mmoja mzungu.

Muitaliano mwenye umri wa miaka 32 amekamatwa kwa tuhuma za mauaji na wizi na mwathiriwa amejulikana kwa jina la Alika Ogorchukwu, baba aliyeoa na mwenye watoto wawili.

Mke wake, aliyetajwa kwa jina la Charity Oriachi, alishindwa kuzuia machozi yake alipokuwa akiviambia vyombo vya habari jinsi alivyoonyeshwa mwili wa mumewe ukiwa umelala chini.

Siku ya Jumamosi mamia ya watu kutoka jamii ya eneo la Nigeria waliingia katika mitaa ya Civitanova Marche, katika mkoa wa Marche, kudai haki huku shambulio hilo likilaaniwa na wanasiasa wa Italia.

#ChanzoBBC

Latest News

RAIS WA UKRAINE AAMURU RAIA WOTE KUHAMA MKOA WA DONETSK.
31 Jul 2022 17:17 - Grace Melleor

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameamuru raia wote ambao bado wanaishi katika maeneo ya mashariki mwa mkoa wa Donetsk [ ... ]

KIFO CHA RAIA WA NIGERIA NCHINI ITALIA CHAZUA HASIRA.
31 Jul 2022 16:58 - Grace Melleor

Kifo cha mhamiaji aliyeshambuliwa mchana kweupe nchini Italia kimezua hasira.

VUTA N’KUVUTE YA MANARA NA KATIBU WA TFF YAIBUKA.
25 Jul 2022 16:37 - Grace Melleor

Katibu Mkuu wa Shrikishi la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Kidao Wilfred amesema amesekitishwa na madai ya yaliyekuwa Af [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.