Star Tv

Katibu Mkuu wa Shrikishi la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Kidao Wilfred amesema amesekitishwa na madai ya yaliyekuwa Afisa wa klabu ya Yanga Haji Manara kuwa alimuomba msamaha kwa maelezo Rais wa TFF Wallace Karia alifanya makosa.

Kidao amesema maneno hayo si ya kweli na Sekretarieti ya TFF haina nafasi ya kuendelea kuzungumzia jambo ambalo tayari limeshatolewa uamuzi na chombo huru cha TFF.

Mapema leo Julai 25, 2022 Manara alizungumza na waandishi wa habari na kusema kwamba aliomba msamaha na pia amekanusha kuwa hakumtolea neno lolote baya Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu na kutaka kamati huru ya uchunguzi iundwe kuchunguza suala hilo na ikiwa atathibitika ni kweli alimtukana Karia anakubali kufungwa jela miaka 10.

Aidha, Julai 21 mwaka huu Kamati ya Maadili ya TFF ilimfungia Manara kujihusisha na mpira wa miguu ndani na nje ya nchi kwa miakamiwili na kupiga faini ya shilingi milioni 20 kwa kosa la kumtishia na kumdhalilisha Rais wa TFF.

Latest News

RAIS WA UKRAINE AAMURU RAIA WOTE KUHAMA MKOA WA DONETSK.
31 Jul 2022 17:17 - Grace Melleor

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameamuru raia wote ambao bado wanaishi katika maeneo ya mashariki mwa mkoa wa Donetsk [ ... ]

KIFO CHA RAIA WA NIGERIA NCHINI ITALIA CHAZUA HASIRA.
31 Jul 2022 16:58 - Grace Melleor

Kifo cha mhamiaji aliyeshambuliwa mchana kweupe nchini Italia kimezua hasira.

VUTA N’KUVUTE YA MANARA NA KATIBU WA TFF YAIBUKA.
25 Jul 2022 16:37 - Grace Melleor

Katibu Mkuu wa Shrikishi la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Kidao Wilfred amesema amesekitishwa na madai ya yaliyekuwa Af [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.