Polisi wa Kenya katika mji mkuu Nairobi wamevamia ofisi zinazoaminika kuwa na uhusiano na naibu wa rais wa nchi hiyo, William Ruto, ambaye ni mmoja wa wagombea wakuu katika uchaguzi wa mwezi ujao.
Afisa wa polisi amesema wapelelezi wamekamata kompyuta mbili na seva mbili.
Aidha afisa katika sekretarieti ya kampeni ya naibu rais ameiambia BBC kwamba hawatataka kuvutiwa na kile alichokitaja kuwa "maonyesho tu kwa umma na usumbufu’’.
Uvamizi huo unajiri huku kukiwa na mvutano kati ya vikosi vya usalama nchini na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini (IEBC).
Mwishoni mwa juma mkuu wa tume hiyo alikosoa vikali uamuzi wa kuwazuilia raia watatu wa kigeni ambao walikuwa wamepewa kandarasi ya kufanyia kazi mfumo wa kielektroniki wa kupiga kura nchini.
#ChanzoBBCSwahili