Star Tv

Binti aliyefahamika kwa jila la Halima Yunusa Ibrahim amempeleka babamkwe wake latika Mahakama ya Kiislamu Islamic (Sharia Court) katika jimbo la Kaduna nchini Nigeria kwa madai ya kukataa aolewe na mpenzi wake Bashir Yusuf.

Taarifa iliyochapishwa na gazeti la The Daily Trust nchini Nigeria limeripoti kwamba Halima aliiambia mahakama kuwa amependana na mpenzi wake Yusuf lakini baba yake Yusuf amekataa asimuoe.

Baba yake Ibrahim, aliiambia mahakama kwamba alikuwa anafahamu kuhusu mapenzi baina ya binti yake na Yusuf, lakini alikuwa hajatimiza vigezo vya kuoa.

Baba huyo alidai kuwa alimwambia mchumba wa binti yake kwamba alikuwa amemtuma awalete wazazi wake lakini hakurudi tena kwa takriban mwaka mmoja.

Alijitokeza baada ya mwaka mmoja baadaye na akamchukua binti yake na wakapotea kwa siku tatu bila kurudi nyumbani ambapo baadaye waliambiwa kuwa walikuwa wameenda kwa shangazi yao, mzee Ibrahim aliiambia mahakama.

Amesema kuwa baadaye walipelekwa katika kituo cha polisi ambako walikamatwa na kupatikana na hatia na baadaye wakaachiliwa kutoka kwenye kituo cha polisi na kutoroka hadi katika mji wa Abuja.

Jaji baada ya kusikia hoja zao, alimuamrisha baba yake Yusuf kumruhusu kijana wake amuoe Halima na iwapo hatofanya hivyo mahakama itawafungisha ndoa.

#ChanzoGazetiDailyTrust
#ChanzoBBC

Latest News

RAIS WA UKRAINE AAMURU RAIA WOTE KUHAMA MKOA WA DONETSK.
31 Jul 2022 17:17 - Grace Melleor

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameamuru raia wote ambao bado wanaishi katika maeneo ya mashariki mwa mkoa wa Donetsk [ ... ]

KIFO CHA RAIA WA NIGERIA NCHINI ITALIA CHAZUA HASIRA.
31 Jul 2022 16:58 - Grace Melleor

Kifo cha mhamiaji aliyeshambuliwa mchana kweupe nchini Italia kimezua hasira.

VUTA N’KUVUTE YA MANARA NA KATIBU WA TFF YAIBUKA.
25 Jul 2022 16:37 - Grace Melleor

Katibu Mkuu wa Shrikishi la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Kidao Wilfred amesema amesekitishwa na madai ya yaliyekuwa Af [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.