Mwili wa Rais wa zamani wa Kenya wa tatu Emilio Mwai Kibaki umewasili katika majengo ya Bunge kwa ajili ya kuagwa. Hii leo mwili huo utaagwa na Rais Uhuru Kenyatta, Naibu Rais William Ruto, mawaziri, mabalozi, wakuu wa jeshi na viongozi wengine wakuu wa serikali.
Kesho Jumanne na Jumatano itakuwa zamu ya wananchi wa kawaida kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Hayati Kibaki ndani ya majengo ya bunge la taifa.
Misa ya kitaifa ya kumuaga Hayati Kibaki itafanywa siku ya Ijumaa tarehe 29, Kisha atazikwa Jumamosi Aprili 30 nyumbani kwake huko Othaya Nyeri.