Star Tv

Rais wa Ukraine Volodynyr Zelensky amesema taifa lake lingefanikiwa kumaliza vita yake na Urusi kama ingekuwa na silaha bora.

Katika hotuba yake ya mara kwa mara katika kanda ya video kwa taifa lake, Rais Zelensky amesema kwamba iwapo Ukraine ilikuwa ikimiliki silaha bora ikilinganishwa na zile za Urusi ingekuwa imemaliza vita.

Amesema kwamba katika mahojiano yake na majadiliano na viongozi wa mataifa yaliopiga hatua kubwa kidemokrasia, "sio haki kwa Ukraine kuendelea kuomba usaidizi wa kile ambacho washirika wake wamekuwa wakihifadhi kwa miaka kadhaa’’.

Amebainisha kwamba iwapo mataifa hayo yanamiliki silaha ambazo Ukraine inahitaji ni jukumu lao kusaidia kulinda na kuokoa maisha ya maelfu ya raia wa Ukraine.

Rais Zelensky ameongezea kwamba iwapo taifa lake lingefanikiwa kupata silaha hizo ambazo wameahidiwa wiki zijazo, zingesaidia kuokoa maisha ya maelfu ya watu kwani uwezo wa mashambulizi ya Urusi katika maeneo ya Kharkiv, Donbasna Dnipropetrovsk umeongezekana hata kulenga makaazi ya raia.

"Hatma ya makumi ya maelfu ya wakaazi wa Mariupol ambao walipelekwa katika maeneo yanayodhibitiwa na Urusi haijulikani’’-Zelensky.

Hatua hii inajiri huku wizara ya ulinzi ya Urusi ikitoa masharti mapya kwa wanajeshi wa Ukraine waliozungukwa katika mji wa Mariupol kusalimu amri.

#ChanzoBBC

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.