Star Tv

Mapigano yameripotiwa kati ya watu wenye silaha na vikosi vya usalama vya Ethiopia katika mji wa Moyale kusini mwa Ethiopia karibu na mpaka wa nchi hiyo na nchi jirani ya Kenya.

Afisa wa eneo hilo ameambia BBC kwamba mapigano hayo yalitokea kati ya Jumamosi jioni na Jumapili asubuhi.

Afisa huyo amesema watu hao waliokuwa na silaha walikuwa wanachama wa kundi la waasi la Oromo Liberation Army (OLA) lakini ameshindwa kufichua iwapo kulikuwa chanzo cha mapigano hayo.

Makubaliano ya kibinadamu yaliyokubaliwa kati ya serikali na vikosi vya Tigray yamezua matumaini ya azimio la vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miezi kumi na saba huko kaskazini. Lakini katika eneo lenye watu wengi zaidi nchini la Oromia mapigano yameendelea kuripotiwa kati ya vikosi vya serikali- ambavyo ni pamoja na jeshi na polisi wa mkoa- na OLA.

OLA kwa upande wao wanasema wanashinda vita. Odaa Tarbii, msemaji wa kundi hilo, amedai katika ujumbe wa Twitter leo Jumatatu kwamba vikosi vya serikali vimewaua waasi wengi katika eneo linaloitwa Malka Lammii kusini mwa Oromia.

Siku ya Jumamosi afisa mkuu wa kijeshi, Kanali Girma Ayele alisema vikosi vya usalama vilikuwa vinachukua hatua dhidi ya OLA katika kile alichokiita "operesheni iliyoratibiwa."
OLA kwa upande wao wanasema wanashinda vita. Odaa Tarbii, msemaji wa kundi hilo, amedai katika ujumbe wa Twitter leo Jumatatu kwamba vikosi vya serikali vimewaua waasi wengi katika eneo linaloitwa Malka Lammii kusini mwa Oromia.

 

Latest News

AMPELEKA MKWE MAHAKAMANI KWA KUMZUIA KUOLEWA.
17 May 2022 06:34 - Grace Melleor

Binti aliyefahamika kwa jila la Halima Yunusa Ibrahim amempeleka babamkwe wake latika Mahakama ya Kiislamu Islamic (Shar [ ... ]

WANAJESHI WA UKRAINE WALIOZINGIRWA WALIOKOLEWA.
17 May 2022 05:50 - Grace Melleor

Ukraine imethibitisha kwamba mamia ya wapiganaji wake waliokuwa wamekwama kwa zaidi ya miezi miwili katika mji wa Maurip [ ... ]

JESHI LA NATO KUANZA KUFANYA MAZOEZI KUKABILI VITA.
16 May 2022 09:23 - Grace Melleor

Mazoezi makubwa zaidi katika historia ya Baltics ya Muungano wa kijeshi wa NATO yanatarajiwa kuanza baadaye hii leo.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.