Star Tv

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza wahandisi wa TARURA wasimamie miradi kwa weledi, uadilifu na uaminifu huku wakizingatia mikataba husika na pia wawe wabunifu kutumia teknolojia mpya, sahihi na rafiki kulingana na upatikanaji wa malighafi za ujenzi.

Amesema hayo leo Februari 12, 2022 alipofungua Mkutano wa Kazi kati ya Ofisi ya Rais - TAMISEMI, TARURA, Wakandarasi, Bodi ya Usajili wa Wakandarasi, Mfuko wa Barabara na Mamlaka ya Ununuzi wa Umma katika Ukumbi wa Mtakatifu Gasper, Dodoma.

“Pia ninaisisitiza TARURA kufanyia kazi haraka, maelekezo ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu kujifunza teknolojia inayotumiwa kutengeneza barabara za Zanzibar ambayo imeonesha kuwa nafuu na ya viwango vya juu.”

Amesema Serikali imefanya jitihada mbalimbali katika kuijengea uwezo TARURA ili iweze kutekeleza makujumu yake ikiwa ni pamoja kuiongezea fedha kutoka sh. bilioni 247.5 ilipoanzishwa mwaka 2017 hadi kufikia Sh. bilioni 752.61 sawa na ongezeko la asilimia 204.3.

“Fedha hizo zinajumuisha sh. bilioni 127.50 kutoka Serikali Kuu, sh. bilioni 272.50 kutoka Mfuko wa Barabara, sh. bilioni 322.15 kutoka katika tozo ya sh. 100 kwa lita ya mafuta ya petroli na dizeli na sh. bilioni 30.44 kutoka kwenye ushuru wa maegesho wa magari.”

Amesema mwaka 2017, TARURA ilikuwa inasimamia mtandao wa barabara wenye urefu wa kilomita 108,946.19 na sasa mtandao huo umeongezeka na kufikia kilomita 144,429.77 ambazo zimetangazwa rasmi kwenye Gazeti la Serikali Na. 463 la tarehe 25 Juni 2021.

Majaliwa ameongeza kuwa wakati TARURA inaanzishwa mwaka 2017, barabara za lami zilikuwa kilomita 1,449.55 sawa na asilimia 1.30 na sasa ni kilomita 2,473.55 sawa na ongezeko la kilomita 1,024 sawa na asilimia 70.6.

Ameiagiza Ofisi ya Rais-TAMISEMI ifuatilie na kuchukua hatua stahiki kwa Halmashauri zote zitakazoshindwa kutekeleza kazi za matengenezo ya barabara kulingana na mkataba wa makubaliano (Annual Performance Agreement).

Pia, Waziri Mkuu amesema TARURA ianze kutekeleza mpango wa uwekaji taa za barabarani wakati wa ujenzi wa barabara. “Hakikisheni hii inakuwa sehemu ya mkataba wa ujenzi wa barabara zote zinazojengwa, jifunzeni utaratibu huu kutoka TANROADS ambao tayari wanautekeleza”.

Waziri Mkuu amewataka wakandarasi wazawa wajiimarishe katika kazi zao za ujenzi wa barabara ili waweze kufanya kazi yenye ubora, kwa wakati na viwango. 

Latest News

Dkt. Jafo ofisi yake, imekamilisha taratibu zote za kupata Ithibati ya Kitabu ch...
24 Apr 2023 09:38 - Kisali Shombe

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amewasilisha bungeni Hotuba ya Ma [ ... ]

TARI, Ukiruguru kuzindua Kifaa cha kupandia Mbegu cha Rafiki
23 Apr 2023 18:33 - Kisali Shombe

Sekta ya Kilimo ni mhimili wa uchumi wa Tanzania na imekuwa ikichangia Pato la mkulima mmoja mmoja, kaya na Taifa kwa uj [ ... ]

Wanawake kuwa sehemu ya Elimu dhidi ya Itikadi Kali na Ugaidi Afrika.
17 Apr 2023 10:28 - Kisali Shombe

Mnamo Oktoba 14, 2017, Mogadishu, Somalia ilikumbwa na shambulio baya la kigaidi lililoua watu 587 na kujeruhi zaidi ya  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2023 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.