Star Tv

Mtangazaji mashuhuri wa BBC Zuhura Yunus anaondoka kutoka shirika hilo baada ya kulitumikia kwa takriban miaka 14.

Zuhura atatangaza kipindi chake cha mwisho cha Dira ya Dunia leo Januri 14, 2022 majira ya saa tatu Afrika mashariki. Hata hivyo taarifa kutoka shirika hilo imeabinisha kuwa Zuhura amebakiza siku kadhaa za likizo kabla ya kuondoka rasmi.

Mtangazaji huyo aliyejiunga na BBC Swahili mwaka 2008 amesema anataka kuutumia muda wake sasa kuendelea na uandishi na mambo mengine nje ya BBC.

Taarifa ya Zuhura kuondoka BBC inakuja miezi kadhaa baada ya kuandika kitabu chake cha wasifu wa Biubwa Amour Zahor mwanaharakati mwanamke wa kisiasa wakati wa mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964.

Zuhura alianza kama mtangazaji wa redio na mzalishaji wa vipindi mwaka 2008. Mwaka 2014 alihamia Swahili TV na akawa mwanamke wa kwanza kutangaza Dira ya Dunia TV.

 

Latest News

AMPELEKA MKWE MAHAKAMANI KWA KUMZUIA KUOLEWA.
17 May 2022 06:34 - Grace Melleor

Binti aliyefahamika kwa jila la Halima Yunusa Ibrahim amempeleka babamkwe wake latika Mahakama ya Kiislamu Islamic (Shar [ ... ]

WANAJESHI WA UKRAINE WALIOZINGIRWA WALIOKOLEWA.
17 May 2022 05:50 - Grace Melleor

Ukraine imethibitisha kwamba mamia ya wapiganaji wake waliokuwa wamekwama kwa zaidi ya miezi miwili katika mji wa Maurip [ ... ]

JESHI LA NATO KUANZA KUFANYA MAZOEZI KUKABILI VITA.
16 May 2022 09:23 - Grace Melleor

Mazoezi makubwa zaidi katika historia ya Baltics ya Muungano wa kijeshi wa NATO yanatarajiwa kuanza baadaye hii leo.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.