Star Tv

Panya maarufu na shujaa wa Tanzania aliyetumika kutafuta na kutegua mabomu ya ardhini na vilipuzi kwa jina la Magawa amefariki dunia mwishoni mwa wiki hii.

Kupitia taarifa iliyotolewa katika ukurasa wa instagram wa shirika la Apopo limesema Magawa alikuwa na afya njema wiki iliyopita lakini afya yake ilianza kudhoofika mwishoni mwa wiki na kuaga dunia akiwa na umri wa miaka minane.

Panya huyo alisifika sana kwa kusaidia kugunduliwa kwa Zaidi ya mabomu 100 ya kutegwa ardhini nchini Cambodia.

"Mchango wake unaruhusu jamii nchini Cambodia kuishi, kufanya kazi na kucheza; bila hofu ya kupoteza maisha au kiungo. Mnamo Septemba 2020, alikabidhiwa rasmi Medali ya Dhahabu ya PDSA - tuzo ya juu zaidi ya ushujaa ambayo mnyama anaweza kupokea. Mwaka jana wakati Magawa alipostaafu, HeroRAT Ronin alichukua kijiti kama panya mpya wa kuasili"- Imebainishwa katika sehemu ya taarifa iliyotangaza kifo cha panya huyo.

#ChanzoBBCSwahili

Latest News

RAIS WA UKRAINE AAMURU RAIA WOTE KUHAMA MKOA WA DONETSK.
31 Jul 2022 17:17 - Grace Melleor

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameamuru raia wote ambao bado wanaishi katika maeneo ya mashariki mwa mkoa wa Donetsk [ ... ]

KIFO CHA RAIA WA NIGERIA NCHINI ITALIA CHAZUA HASIRA.
31 Jul 2022 16:58 - Grace Melleor

Kifo cha mhamiaji aliyeshambuliwa mchana kweupe nchini Italia kimezua hasira.

VUTA N’KUVUTE YA MANARA NA KATIBU WA TFF YAIBUKA.
25 Jul 2022 16:37 - Grace Melleor

Katibu Mkuu wa Shrikishi la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Kidao Wilfred amesema amesekitishwa na madai ya yaliyekuwa Af [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.