Star Tv

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri huku akiteua mawaziri wapya watano.

Akitangaza mabadiliko hayo leo Jumamosi Januari 8, 2022 Ikulu jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Kattanga amesema Rais amefanya mabadiliko ya muundo katika wizara tatu.

Mawaziri wapya watano walioteuliwa ni; Nape Nnauye (Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari), Hamad Masauni (Mambo ya Ndani), Dkt. Pindi Chana (Sera Bunge na Uratibu), Anjelina Mabula (Ardhi) na Husein Bashe (Kilimo).

Pia Rais Samia ameteua manaibu waziri wapya katika wizara tano.

Manaibu waziri hao wapya walioteuliwa ni pamoja na; Anthony Mavunde (Kilimo), Jumanne Sagini (Mambo ya Ndani) Dkt. Lemomo Kiruswa (Madini), Ridhiwani Kikwete (Ardhi) na Atupele Mwakibete (Ujenzi na Uchukuzi).

Pia, Rais Samia amewabadilisha na kuwahamisha mawaziri katika wizara tisa.
Rais Samia ''ameunganisha wizara tatu, iliyokuwa wizara ya uwekezaji iliyokuwa chini ya ofisi ya Waziri Mkuu na pia ameunganisha wizara ya biashara moja ambayo itaitwa uwekezaji, viwanda na biashara'', amesema Balozi Hussein Kattanga.

Aidha kama alivyoahidi Rais Samia ameunda Wizara ya Maendeleo ya jamii, jinsia,wanawake na Makundi maalum.

Wizara maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum, wizara hii itaongoozwa na Waziri Dorothy Gwajima ambaye alikuwa waziri wa Afya.

Wizara mpya ya Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalum, itaaongoozwa na Waziri Dorothy Gwajima ambaye alikuwa waziri wa Afya.

Kulingana na mabadiliko hayo, Wizara ya katiba na sheria imepata waziri mpya George Simbachawene ambaye amechukua wadhifa wa Profesa Palamagamba Kabudi.

Wizara ya Habari na teknolojia ya habari pia itaongozwa na Waziri mpya aliyekuwa Waziri wa zamani Nape Moses Nnauye.

Kulingana na Balozi Kattanga, Rais Samia amefanya mabadiliko pia katika nafasi za makatibu wakuu na Manaibu katibu wakuu.

Wizara ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora itaongozwa na Waziri mpya Jenista Mhagama ambaye amehamishwa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera, Bunge, Kazi, Ajira Vijana na watu wenye Ulemavu.

Aliyekuwa Waziri wa Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mohamed Mchengerwa atakuwa Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Kuchukua nafasi ya Inocent Bashungwa.

Innocent Bashungwa, anakuwa Waziri mpya wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Ummy Mwalimu, aliyehamishiwa Wizara ya Afya.

Mawaziri waliobakia katika nafasi zao ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberatha Mulamula; Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba; Waziri wa Nishati, January Mkamba; Waziri wa Madini, Doto Biteko; Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro; Waziri wa Maji, Jumaa Aweso; Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa; Waziri wa Ulinzi, Stegomena Tax; na Waziri Ofisi ya Rais - Kazi Maaalum, George Mkuchika.

Latest News

MATETEMEKO MAWILI YA ARDHI YAUA WATU 22 AFGHANISTAN.
18 Jan 2022 09:36 - Grace Melleor

Takriban watu 22 wafariki kufikia sasa baada ya matetemeko ya ardhi ya mfululizo kukumba magharibi mwa Afghanistan siku  [ ... ]

WAZIRI MKUU AWATAKA MABALOZI KUVUTIA WAWEKEZAJI.
17 Jan 2022 16:24 - Grace Melleor

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika mataifa mbalimbali watoe msukumo Katika u [ ... ]

RAIS WA MALI ALIYEPENDULIWA MADARAKANI AFARIKI.
17 Jan 2022 06:53 - Grace Melleor

Rais wa Mali aliyeondolewa madarakani Ibrahim Boubacr Keita amefariki akiwa na umri wa miaka 76, familia yake na rafiki  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.