Star Tv

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango leo tarehe 18 Novemba 2021 ametembelea Bandari ya nchi ya Singapore na kujionea namna inavyofanya kazi.

Katika ziara hiyo Makamu wa Rais ameshuhudia teknolojia mbalimbali zinazotumika katika kufanya kazi katika bandari hiyo ikiwemo upakuaji na upakiaji makasha na mizigo, ukaguzi wa mizigo pamoja na ufuatiliaji makasha wakati wote yanapokuwa safarini.

Akitoa maelezo namna bandari hiyo ilivyopiga hatua kubwa katika kipindi cha muda mfupi Makamu wa Rais wa Mamlaka ya Bandari ya Singapore anayeshugulikia masuala ya biashara bwana Ong Seow Leong amesema bandari hiyo imewekeza katika mafunzo pamoja na ubunifu uliopelekea kuongezeka kwa teknolojia inayotumika hivi sasa katika kutoa huduma ikiwemo kuweza kufanikiwa kushusha na kupakia makasha laki moja ndani ya siku moja.

Amesema bandari ya Singapore imekuwa na mtandao na bandari zingine duniani hivyo kuongeza ufanisi wa ufanyaji kazi wa bandari hiyo.

Aidha ameongeza kwamba Bandari ya Singapore imekuwa ikiweka mkazo katika kutafuta masoko pamoja na kufanya tafiti zinazoweza kuongeza watumiaji wa bandari hiyo.

Katika hatua nyingine Bwana Leong ameeleza kuwa ni lazima kuwepo na mipango ya muda mrefu katika uendeshaji wa bandari na tayari nchi ya Singapore inaendelea na ujenzi wa bandari mpya na ya kisasa ambayo kwa miaka ijayo itaweza kutoa huduma kwa ufanisi zaidi.

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amesema Tanzania itashirikiana na Uongozi wa Bandari ya Singapore katika kutoa mafunzo kwa watumishi wa bandari za Tanzania pamoja na kupeleka watalaamu wa bandari kutoka Singapore kwenda Tanzania ili kushirikiana katika kufanya maboresho ya haraka hasa katika bandari ya Dar es salaam.

 

Latest News

SHAMBULIO LA KUJITOA MHANGA LAUA WATU NANE SOMALIA.
25 Nov 2021 10:26 - Grace Melleor

Polisi nchini Somalia wamethibitisha vifo vya raia katika bomu lililotegwa ndani ya gari katika mji mkuu Mogadishu, tele [ ... ]

WAZIRI MKUU SWEDEN AJIUZULU SAA CHACHE BAADA YA KUTEULIWA.
25 Nov 2021 09:01 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke kuwahi kushikilia wadhifa huo nchini Sweden amejiuzulu saa chache mara baada ya kuteuliwa [ ... ]

MTOTO WA GADDAFI AZUIWA KUGOMBEA URAIS LIBYA.
25 Nov 2021 07:13 - Grace Melleor

Mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa Libya hayati Muammar Gaddafi ameenguliwa katika kinyang’anyiro cha kuwania uchaguzi wa  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.