Star Tv

Rais wa mwisho mzungu wa Afrika Kusini FW de Klerk, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 85 wiki iliyopita, atazikwa katika sherehe ya faragha siku ya Jumapili, kulingana na wakfu wake.

Taarifa iliyotolewa na Familia yake ilibainisha kuwa, “Wakfu wa FW de Klerk unawatangazia kuwa kuchomwa kwa FW de Klerk’ na mazishi yake itafanyika Jumapili Novemba, 2021,”.

“Itakua shere ya faragha kwa familia na haitakua wazi kwa vyombo vya habari,”- Wakfu huo uliongeza na hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa.

De Klerk aliingia madarakani mwaka 1989 chini ya utawala wa ubaguzi wa rangi, mfumo ambao ulihalalisha ubaguzi wa rangi, lakini baadaye akawa mtu muhimu katika kipindi cha mpito kuelekea demokrasia.

Mwaka 1993, alipata Tuzo ya Amani ya Nobel na rais wa zamani Nelson Mandela kwa kusaidia kujadili kukomesha ubaguzi wa rangi.

Alifariki Alhamisi baada ya kupatikana na saratani mapema mwaka huu.

#ChanzoBBC

Latest News

SHAMBULIO LA KUJITOA MHANGA LAUA WATU NANE SOMALIA.
25 Nov 2021 10:26 - Grace Melleor

Polisi nchini Somalia wamethibitisha vifo vya raia katika bomu lililotegwa ndani ya gari katika mji mkuu Mogadishu, tele [ ... ]

WAZIRI MKUU SWEDEN AJIUZULU SAA CHACHE BAADA YA KUTEULIWA.
25 Nov 2021 09:01 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke kuwahi kushikilia wadhifa huo nchini Sweden amejiuzulu saa chache mara baada ya kuteuliwa [ ... ]

MTOTO WA GADDAFI AZUIWA KUGOMBEA URAIS LIBYA.
25 Nov 2021 07:13 - Grace Melleor

Mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa Libya hayati Muammar Gaddafi ameenguliwa katika kinyang’anyiro cha kuwania uchaguzi wa  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.