Star Tv

Makamu wa Rais wa Tanzania amemuagiza Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Dkt. Festo Dugange kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu Hamis Dambaya ili kupisha uchunguzi kutoka vyombo husika.

Dkt. Mpango, amefika uamuzi huo leo Julai 24, 2021 mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika stendi ya Mabasi ya Mangaka iliopo Wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara.

Makamu wa Rais amekasirishwa na uongozi wa Wilaya kufanya upotevu wa fedha usiolingana na matokeo ya ujenzi wa mradi huo.

Ujenzi wa majengo ya stendi hiyo umetumia Shilingi Bilioni 2.2 kiasi ambacho Makamu wa Rais amesema hakilingani na ujenzi huo.

“Unajua vitu vingine Mkurugenzi ukiona huwezi kazi hii awamu ya sita jiondoe mwenyewe, Kwasababu hili jengo la hii stendi halijatumia hizo zaidi ya Shilingi Bilioni mbili unazonitamkia....lakini nitakufuatilia mpaka hela ipatikane…alafu unasema uongo na hela za maskini hawa. Hizo hela zirejeshwe kwasababu kinachooneka ni wakandarasi wanachezea hili jengo, anza kushughulika naye”- Ameagiza Makamu wa Rais Dkt. Mpango.

Aidha, Dkt. Mpango amesema viongozi hawana budi kusimamia fedha za serikali zinazopelekwa katika maeneo yao ili kuwaletea maendeleo wananchi na si vinginevyo.

Latest News

KENYA YAPIGA MARUFUKU FILAMU YA WAPENZI WA JINSIA MOJA.
23 Sep 2021 14:44 - Grace Melleor

Bodi ya Filamu Kenya inasema kuwa filamu kuhusu maisha ya wanandoa wa jinsia nchini Kenya imepigwa marufuku nchini humo. [ ... ]

SHIL. MIL. 700 ZATOLEWA KUKARABATI BARABARA KARAGWE.
23 Sep 2021 13:55 - Grace Melleor

Serikali imetoa Shilingi Milioni 700 kusaidia ukarabati wa barabara za vijijini katika jimbo la Karagwe mkoani Kagera il [ ... ]

BABA AKAMATWA KWA KUCHOMA 'MATITI' YA BINTI YAKE.
22 Sep 2021 13:32 - Grace Melleor

Polisi katika jimbo la Nigeria la Lagos wamemtia nguvuni mwanaume mmoja kwa madai ya kuyaondoa matiti ya binti yake mwen [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.