Rais wa Marekani Joe Biden amemhakikishia Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani msaada wa kidiplomasia na kiutu wakati kundi la Taliban likiendelea kuiwekea shinikizo serikali inayoungwa mkono na Marekani huko Kabul.
Katika mazungumzo ya njia ya simu Biden na Ghani wamekubaliana kwamba mashambulizi ya sasa ya Kundi la Taliban yanapingana na harakati ya kudai kuunga mkono mazungumzo ya kutatua mgogoro wa eneo hilo.
Biden hapo jana Julai 23, ameidhinisha Dola Milioni100 katika kushughulikia suala la wakimbizi wa Afghanistan.
Fedha hizo pia zitawasaidia wale wanaoomba visa maalumu, ambapo karibu raia 20,000 wa Afghanistan walikuwa wakifanya kazi ya ukalimani kuisadia Marekani wakati wa vita na sasa wanahofia kuadhibiwa na Taliban.
#ChanzoDWSwahili