Star Tv

Raia kadhaa wa mataifa ya kigeni pamoja na wengine wa nchini Madagascar wanashikiliwa na mamlaka nchini humo kwa tuhuma za jaribio la mauaji ya Rais Andry Rajoelina.

Mwanasheria mkuu wa serikali nchini humo amesema kwenye taarifa yake kwamba raia wawili wa Ufaransa ni miongoni mwa waliokamatwa.

Watu hao kadhaa wamekamatwa kwa kutaka kumuua Rais wa Taifa hilo la Kisiwa ikiwa ni sehemu ya uchunguzi unaohusiana na kudhoofisha hali ya usalama wa taifa hii pia ikiwa ni kulingana na duru za kidiplomasia.

Rajoelina alikula kiapo cha Urais mwaka 2019 baada ya uchaguzi mgumu ambao ulipingwa kwenye mahakama ya kikatiba kutoka kwa wapinzani wake.

#ChanzoBBCSwahili

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.