Star Tv

Afrika Kusini imepeleka jeshi kukabiliana na ghasia zilizotokea baada ya kufungwa kwa Rais wa zamani wa taifa hilo Jacob Zuma.

Maduka yalivamiwa na majengo yalichomwa moto siku ya Jumatatu, wakati Zuma akisikiliza kesi yake katika mahakama ya juu.

Watu wapatao sita wameuawa na 200 kukamatwa tangu ghasia hizo zianze wiki iliyopita.

Zuma amehukumiwa kwa kosa la kuidharau mahakama baada ya kushindwa kuhudhuria kesi yake ya madai ya rushwa wakati wa utawala wake.

Zuma mwenye umri wa miaka 79, ambaye alikanusha kuhusika katika madai ya rushwa, lakini alienda mwenyewe polisi wiki iliyopita ili kuanza kifungo chake cha miezi 15.

Kesi hiyo imeibua matukio ambayo hayakutarajiwa nchini humo ambapo hawajawahi kushuhudia kuona Rais wa zamani akifungwa gerezani.

Jumatatu hii Julai 12, 2021 picha za video zilionesha maduka makubwa yakichomwa moto katika mji wa Pietermaritzburg, katika eneo alikotokea Zuma, KwaZulu-Natal, na watu wakifanya maandamano.

Jumapili waandamanaji walionekana wakiandamana katika maeneo ya biashara ya mjini Johannesburg.

Jeshi limesema limeagizwa kwenda kusaidia kupunguza ghasia ambazo zimekuwa zikiendelea kwa siku kadhaa.

Rais Cyril Ramaphosa amesisitiza raia wanaoandamana kuwa na utulivu akisema hakuna maelezo juu ya vurugu hizo.

Zuma alikamatwa kawa kukaidi maelezo ya kutoa ushaidi juu ya kesi ya rushwa ilyokuwa inamkabili wakati yuko madarakani.

Latest News

SHAMBULIO LA KUJITOA MHANGA LAUA WATU NANE SOMALIA.
25 Nov 2021 10:26 - Grace Melleor

Polisi nchini Somalia wamethibitisha vifo vya raia katika bomu lililotegwa ndani ya gari katika mji mkuu Mogadishu, tele [ ... ]

WAZIRI MKUU SWEDEN AJIUZULU SAA CHACHE BAADA YA KUTEULIWA.
25 Nov 2021 09:01 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke kuwahi kushikilia wadhifa huo nchini Sweden amejiuzulu saa chache mara baada ya kuteuliwa [ ... ]

MTOTO WA GADDAFI AZUIWA KUGOMBEA URAIS LIBYA.
25 Nov 2021 07:13 - Grace Melleor

Mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa Libya hayati Muammar Gaddafi ameenguliwa katika kinyang’anyiro cha kuwania uchaguzi wa  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.