Star Tv

Mahakama nchini Afrika Kusini imemhukumu kifungo cha miezi 15 aliyekuwa rais wa taifa hilo, Jacob Zuma.

Hii ni baada ya Korti ya Katiba kumpata na hatia ya kukaidi agizo la kufika mahakamani baada ya kukosa kufika kwenye kikao cha uchunguzi wa kesi ya ufisadi wakati alipokuwa rais.

Mahakama ilikuwa na jukumu la kuamua kama Bw. Zuma anapaswa kuadhibiwa kwa kukataa wito wa mahakama na amri ya mahakama ya kumtaka afike mahakamani kutoa ushahidi kuhusu shutuma za rushwa wakati wa utawala wake.

Mwenyekiti wa kamati maalum ya uchunguzi wa mahakama, Raymond Zondo ambayo imekuwa ikichunguza madai hayo aliiomba mahakama itamke kuwa rais huyo wa zamani alidharau mahakama na imhukumu kifungo cha miaka miwili.

Tangu alipojiuzulu mnamo mwaka 2018, Bwana Zuma amekuwa akifika mahakamani kwa kukabiliwa na shutuma za ufisadi ambazo amekuwa akizikanusha.

Wafanyabiashara walishutumiwa kwa kula njama na wanasiasa kushawishi mchakato wa kufanya maamuzi ya serikali Rais huyo wa zamani alijitokeza mara moja kwenye uchunguzi wa kile kilichojulikana kama kukamatwa kwa serikali lakini akakataa kujitokeza baadaye.

Uchunguzi huo ulioongozwa na Jaji Raymond Zondo uliuliza Korti ya Katiba iingilie kati.

Aidha haijajulikani bado ikiwa Bwana Zuma sasa atakamatwa au Laah.

Katika suala tofauti la kisheria, Bwana Zuma alikataa hatia mwezi uliopita katika kesi yake ya ufisadi iliyohusisha makubaliano ya silaha ya $ 5bn (£ 3bn) kutoka miaka ya 1990.

#ChanzoBBCSwahili

Latest News

“MAISHA HAYAJI MARA MBILI, TUSIPOTOSHE KUHUSU CHANJO”-IGP. Simon Sirro.
29 Jul 2021 11:30 - Grace Melleor

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP. Simon Sirro, amewataka Wananchi na Watanzania kwa ujumla wasidanganywe na watu wacha [ ... ]

“MIMI NI MAMA, BIBI, MKE NA RAIS, SIWEZI KUJIWEKA KATIKA HATARI”-Rais Samia....
28 Jul 2021 10:26 - Grace Melleor

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amepokea chanjo dhidi ya Ugonjwa wa COVID-19, Ambayo ameizindua leo Julai 28, Katik [ ... ]

MSICHANA AUAWA KWA KUVAA JEANS.
28 Jul 2021 09:51 - Grace Melleor

Msichana mmoja aliyejulikana kwa jina la Neha Paswan, mwenye umri wa miaka 17, anadaiwa kupigwa hadi kufa na watu wa fam [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.