Star Tv

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Gutterres amesema maeneo kadhaa katika jimbo la Tigray Kaskazini mwa Ethiopia yanakabiliwa na tisho la baa la njaa.

Gutterres ameonya, kwa kusema kuwa hali inaendelea kuwa mbaya zaidi endapo ufadhili hautaongezwa na njia za kufikia walioathiriwa haitaimarishwa.

''Hatua tunazochukua sasa zinaweza kuwaokoa watu wengi walio katika hatari ya kuangamia kutokana na ukosefu wa chakula"- alisema Gutterres.

Wakazi wa Magharibi mwa Tigray wameiambia BBC kwamba hawana chakula na kwamba wanakabiliwa na baa la njaa.

Watu wa wilaya ya Qafta Humera waliofikiwa kwa nji aya simu wamesema majambazi wamevamia mashamba yao na kuchukua mifugo yao.

Mark Lowcock ameiambia BBC kwamba mamia ya watu tayari wanakabiliwa na njaa katika eneo la Tigray kufuatia miezi kadhaa ya mapigano.

Mamlaka nchini Ethiopia inasisitiza kwamba hali ya utulivu imerejeshawa katika eneo hilo na njia za kuwafikia wakazi kufunguliwa.

Lakini UN inasema maelfu ya watu sasa wanaelekea kukabiliwa na baa la njaa kama lile lililoshuhudiwa mwaka 1984.

Mzozo ulizuka Tigray mwezi Novemba baada ya serikali ya Ethiopia kuanzisha oparesheni ya kijeshi ya kuondoa mamlakani chama tawala cha zamani TPLF, baada ya wapiganaji wake kuteka kambi za jeshi la muungano.

Latest News

WATANZANIA WATAKIWA KUENDELEA KULIPA KODI BILA KUCHOKA.
14 Jun 2021 19:01 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka watanzania kuendelea kujitoa kulipa kodi ili kuwez [ ... ]

WAZIRI MKUU MPYA AAPA KUIUNGANISHA ISRAEL.
14 Jun 2021 06:33 - Grace Melleor

Waziri Mkuu mpya wa Israel Naftali Bennett ameapa kuliunganisha taifa hilo ambalo linalezwa kufadhaishwa na chaguzi nne  [ ... ]

RAIS SAMIA AZINDUA KIWANDA CHA KUSAFISHA DHAHABU NA JENGO LA BOT.
13 Jun 2021 14:11 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amezindua kiwanda cha kusafisha dhahabu jijini Mwanza kinach [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.