Star Tv

Rais wa Syria Bashar al-Assad ameshinda muhula wa nne madarakani kwa kupata asilimia 95.1 ya kura zote zilizopigwa.

Vyama vya upinzani Syria pamoja na mataifa ya Magharibi vimemkosoa Assad na kusema kwamba uchaguzi huo ulitawaliwa na udanganyifu. Serikali ya Assad imesema uchaguzi uliofanywa Jumatano unaonyesha kwamba Syria inaendesha shughuli zake kikamilifu licha ya mgogoro wa mwongo mzima. Vita hivyo vimesababisha vifo vya mamia kwa maelfu ya watu na wengine milioni 11 ambao ni nusu ya idadi ya watu kupoteza makazi yao. Spika wa bunge Hammouda Sabbagh alitangaza matokeo katika mkutano wa waandishi wa habari jana, na kusema kwamba asilimia 78 ya watu walijitokeza kupiga kura ambayo ni zaidi ya Wasyria milioni 14.

CHANZO: IDHAA YA KISWAHILI (DW)

Latest News

WATANZANIA WATAKIWA KUENDELEA KULIPA KODI BILA KUCHOKA.
14 Jun 2021 19:01 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka watanzania kuendelea kujitoa kulipa kodi ili kuwez [ ... ]

WAZIRI MKUU MPYA AAPA KUIUNGANISHA ISRAEL.
14 Jun 2021 06:33 - Grace Melleor

Waziri Mkuu mpya wa Israel Naftali Bennett ameapa kuliunganisha taifa hilo ambalo linalezwa kufadhaishwa na chaguzi nne  [ ... ]

RAIS SAMIA AZINDUA KIWANDA CHA KUSAFISHA DHAHABU NA JENGO LA BOT.
13 Jun 2021 14:11 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amezindua kiwanda cha kusafisha dhahabu jijini Mwanza kinach [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.