Baraza la Mawaziri nchini Ethiopia limetaja chama Tawala cha zamani cha Tigray Peoples Liberation Front (TPLF) party na kundi la Oromo Shene kama makundi ya kigaidi, Shirika la utangazaji wa Fana limeripoti.
Serikali ya nchini humo imelaumu mashirika hayo kwa kuhusika na mashambulio yaliofanywa katika maeneo tofauti yakiwalenga raia kwa lengo la kulemaza mageuzi yaliyoanzishwa na nchini humo katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
Mwezi Novemba mwaka jana, Ethiopia ilianzisha oparesheni ya kijeshi Kaskazini mwa Jimbo la Tigray kuondoa madarakani TPLF kufuatia shambulio dhidi ya kambi za kijeshi katika eneo hilo.
Aidha, wakati Ethiopia inajiandaa kufanya uchaguzi mwezi Juni mwaka huu, Utawala wa Waziri Mkuu Abiy Ahmed umekumbwa na ghasia za kijamii zinazohusishwa na kundi la Shene.