Star Tv

Korea Kaskazini imepuuza wazo la kufanya mazungumzo na Marekani siku moja baada ya utawala mjini Washington kusema uko tayari kwa majadiliano ya kidiplomasia kuhusu Pyongyang kuachana na mradi wake wa nyuklia.

Wizara ya mambo ya kigeni ya Korea Kaskazini imesema haiko tayari kufanya mazungumzo na taifa linalotumia diplomasia walizoziita  ni "bandia" kuficha matendo yake ya uchokozi.

Taifa hilo pia limemtahadharisha rais Joe Biden wa Marekani dhidi ya kuchukua kile ilichokitaja kuwa ni "msimamo uliopitwa na wakati" na kuonya kuwa Washington itapata madhara kwa kuichokoza Korea Kaskazini.

Matamshi kutoka Pyongyang yanatolewa siku kadhaa tangu rais Biden alipoliambia bunge la Marekani kuwa utawala wake utatumia diplomasia pamoja na msimamo usioyumba kudhibiti malengo ya nyuklia ya Korea Kaskazini.

Latest News

“TUTAJIRIDHISHA KABLA YA KUKUBALI CHANJO YA CORONA”- Rais Samia.
14 May 2021 18:24 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kabla ya kupokea chanjo ya virusi vya Corona ni lazi [ ... ]

SOMALIA YATANGAZA KUREJESHA UHUSIANO NA KENYA.
06 May 2021 17:57 - Grace Melleor

Somalia imetangaza kuwa inarejesha mahusiano ya kidiplomasia na nchi jirani ya Kenya baada ya kusitisha mahusiano hayo m [ ... ]

KENYA NA TANZANIA KUONDOA VIKWAZO VYA BIASHARA.
05 May 2021 15:39 - Grace Melleor


Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania iko tayari kuwapokea wawekezaji kutoka Kenya pamoja na kuondoa vikwazo visivy  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.