Wasafiri wanaoelekea Ireland kutoka Kenya watalazimika kujitenga kwa wiki mbili baada ya kuwasili katika nchi hiyo ya bara Ulaya.
Siku ya Jumamosi, Dublin iliongeza Kenya na nchi nyingine kadhaa kwenye toleo lake la orodha ya nchi zilizowekea vikwazo vya usafiri kwa ajili ya Covid-19, ambazo wasafiri wake lazima wangeweka mapema hoteli watakazotumia kama karantini.
Maafisa walisema agizo hilo ambalo linaanza kutumika mnamo Aprili 15 linalenga kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona.
Nchi nyingine tano ziliongezwa kwenye orodha huku kukiwa na wasiwasi juu ya aina mpya za Covid-19
Nchi nyingine ni pamoja na Ubelgiji, Ufaransa, Italia, Luxemburg, Marekani , Canada, Bangladesh, Pakistan, Uturuki, Armenia, Bermuda, Bosnia na Herzegovina, CuraƧao, Maldives na Ukraine.
Wasafiri kutoka Kenya watahitajika, kuanzia saa 4 asubuhi Alhamisi hii kujiandikisha katika hoteli zilizotengwa za karantini kwa gharama zao wanapowasili Ireland.
"Mipangilio hii inatumika kwa abiria yeyote ambaye amekuwa katika yoyote ya nchi hizi katika siku 14 zilizopita, hata ikiwa anapitia mojawapo ya nchi hizi na hata ikiwa amebaki barabarani,"- Sehemu ya taarifa kutoka kwa tovuti ya ubalozi wa Ireland imesema.
Chanzo:BBCSwahili