Star Tv

Utawala wa kijeshi nchini Myanmar umeahidi utaitisha uchaguzi na kukabidhi madaraka.

Hata hivyo, utawala huo umekanusha kwamba kitendo cha kuondolewa madarakani serikali iliyochaguliwa na wananchi kilikuwa ni mapinduzi au kwamba viongozi wake walikamatwa na wanawashutumu waandamanaji kwa kuchochea ghasia na vitisho.

Msemaji wa baraza linalotawala, Brigedia Jenerali Zaw Min Tun amesema leo kuwa lengo lao ni kuitisha uchaguzi na kukabidhi madaraka kwa chama kitakachoshinda. Kauli hiyo ameitoa kwenye mkutano wa kwanza na waandishi habari tangu jeshi lilipoiondoa madarakani serikali ya Aung San Suu Kyi.

Jeshi halijatangaza tarehe ya kufanyika uchaguzi mpya, lakini limetangaza hali ya hatari kwa mwaka mmoja. Aidha, Suu Kyi amefunguliwa mashtaka mapya ikiwemo kukiuka sheria ya usimamizi wa majanga ya Myanmar kuhusu hatua za kukabiliana na virusi vya corona.

Wakati huo huo, China imekanusha uvumi kwamba inahusika kwenye mapinduzi ya kijeshi ya Myanmar.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.