Star Tv

Maafisa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamesema zaidi ya watu 60 wamezama baada ya mashua kupinduka na kuzama katika mto Congo.

Mamlaka za nchini humo zimeeleza kuwa watu 300 wameokolewa lakini inakisiwa kuwa watu wengine 200 hawajulikani walipo baada ya ajali hiyo.

Wakazi wanasema boti iligonga mwamba mashariki mwa mji mkuu Kinshasa, wakati walipokuwa wakisafiri usiku.

Safari za majini nyakati za usiku zimepigwa marufuku nchini humo.

Waziri wa masuala ya kibinadamu, Steve Mbikayi, ametaka wale wamiliki wa boti kushtakiwa.

"Chombo kilichojaa kupita kiasi, kilichokuwa na abiria zaidi ya 700 kilipinduka Mai-Ndombe! Miili 60 tayari imepatikana na watu 300 wamenusurika Tunazipa pole familia zilizofiwa na tunataka hatua zichukuliwe dhidi ya wale wote wanaohusika na sekta ya uchukuzi"- aliandika Waziri huyo kwenye mtandao wa Twitter.

Aidha, imeeelezwa kuwa kuna barabara chache nchini DRC na shughuli nyingi za usafiishaji wa mizigo na abiria ambao hufanywa kwa njia ya mto.

Latest News

RAIS MAGUFULI AWAONYA WAKANDARASI WANAOCHELEWESHA MIRADI.
24 Feb 2021 13:33 - Grace Melleor

Rais John Magufuli amezindua barabara ya juu eneo la Ubungo ambayo imepewa jina la Marehemu John Kijazi, ambaye alikuwa  [ ... ]

MWILI WA BALOZI WA ITALIA WASAFIRISHWA KWENDA ROMA.
24 Feb 2021 09:52 - Grace Melleor

Mwili wa balozi wa Italia aliyeuawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika jaribio la utekaji nyara uliotibuka s [ ... ]

MWANASIASA WA UPINZANI WA RWANDA AUAWA.
22 Feb 2021 07:59 - Grace Melleor

Mwanasiasa wa upinzani na raia wa Rwanda anayeishi mafichoni nchini Afrika Kusini ameuawa kwa kupigwa risasi.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.