Waandamanaji dhidi ya ghasia za polisi katika mji mkuu wa Nigeria Abuja wameshambuliwa na wanaume wasiojulikana waliokuwa wamebeba mapanga.
Walioshuhudia tukio hilo wanasema mamia ya waandamanaji kadhaa walikuwa wamekusanyika katika kati ya mji huo wakati shambulio lilipotokea.
Muandamanaji mmoja amesema baadae baadhi ya wavamizi hao walikamatwa na kukabidhiwa kwa maafisa.
Maandamano yamekuwa yakifanyika katika miji mbalimbali kote nchini Nigeria kwa wiki nzima iliyopita.
Ghasia zimeendelea licha ya kuvunjwa kwa kikosi tata cha polisi- cha kukabiliana na wizi kinachofahamika kama SARS.
Aidha, waandamanaji hao wameapa kuendelea kuwepo mitaani mpaka pale haki kamili ya wananchi wa Nigeria itakapopatikana.