Star Tv

Star TV inaungana na Watanzania Wote, ikiwa leo ni kumbukumbu ya miaka 21 ya kifo cha Baba wa taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere aliyefariki 14.10.1999.
Baba wa Taifa Mwl. Nyerere atakumbukwa kwa ukombozi wa Tanzania pamoja na kupigania uhuru wa nchi nyingine za Bara la Afrika.

Kumbukizi hii ya miaka 21 ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ni isiyosahaulika kwa Watanzania pamoja na waafrika kwa ujumla ambao wanatambua mchango wake katika ukombozi wa baadhi ya nchi za bara la Afrika.

Mwl. Nyerere alifariki nchini Uingereza nchini Uingereza alipokuwa anapatiwa matibabu
Mwl. Nyerere ndiye alikuwa Rais wa kwanza wa Tanganyika na aliongoza tangu Taifa lilipopata Uhuru, Desemba 9, 1961 hadi mwaka 1985.

Mbali na nukuu nyingi alizokuwa akizitoa katika hotuba yake na hii ni mojawapo itakumbukwa ikiwa tunaelekea uchaguzi mkuu Oktoba 28;
"Hakuna taifa lenye haki ya kufanya maamuzi kwa ajili ya taifa jingine, hakuna watu kwa ajili ya watu wengine"-Mwl.Nyerere (Ujumbe wa amani wa mwaka mpya nchini, Januari 1968).

#Tuendelee kumuenzi kwa kuziishi hekima na busara zake.
#KumbukiziSikuyaMwalimuNyerere
#Miaka21BilaBabaWaTaifa
#HappyNyerereDay

Latest News

ETHIOPIA YASEMA HAITISHWI NA TAMKO LA RAIS DONALD TRUMP.
24 Oct 2020 16:54 - Grace Melleor

Waziri mkuu wa Ethiopia amesema nchi yake "haitakubali vitisho vya aina yoyote" baada ya Rais Donald Trump kusema kuwa M [ ... ]

RAIS TSHISEKEDI ATANGAZA MASHAURIANO YA UMOJA KWA MUUNGANO TAWALA.
24 Oct 2020 06:41 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi, katika hotuba yake kwa taifa aliyoitoa siku ya Ijumaa wiki hi [ ... ]

SEKTA YA AFYA NCHINI YAPATA NEEMA KUTOKA USWISI.
23 Oct 2020 15:23 - Grace Melleor

Serikali imepokea msaada wa Faranga za Uswisi Milioni 15.75 sawa na shilingi Bilioni 39.59 kwa ajili ya kugharamia mradi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.