Star Tv

Rais wa Marekani Donald Trump amerejea kwa kishindo katika Ikulu ya White House kuendelea na tiba ya virusi vya corona baada ya kulazwa hospitali kwa siku tatu.

Rais  Trump alitoa barakoa yake katika roshani ya White House, ambako wafanyakazi kadhaa na washauri wake walipatikana na virusi hivi karibuni.

Akiwa amevalia suti , tai na barakoa,Trump alitoka nje ya Hospitali ya kitaifa ya kijeshi ya Walter Reed mjini Washington DC Jumatatu usiku akikunja ngumi na kuinua mkono juu.

Maswali bado yanaibuliwa kuhusu ugonjwa wa Bw. Trump baada taarifa kinzani kutolewa wikendi iliyopoti kuhusu hali yake. Ukubwa wa mlipuko wa virusi katika Ikulu ya White House bado unaendelea kuwa kitendawili.

Rais Trump kupitia ukurasa wake wa twitter aliandika "Najihisi vyema sana, Usiogope Covid. Usiache itawale maisha yako."

Zaidi ya watu milioni 7.4 wamethibitishwa kuwa na ugonjwa wa Covid-19 nchini Marekani.

Baada ya safari fupi ya helikopta, RaisTrump alipigwa picha akiwa peke yake kwenye roshani ya Truman katika Ikulu ya White House.

Saa chache baadae, aliweka ujumbe kwenye Twitter kama ishara kwamba anajiandaa kurejea kwenye msururu wa kampeni.

Trump anagombea muhula wa pili madarakani na atakabiliana na mpinzani wake wa chama cha Democratic Joe Biden chini ya mwezi mmoja katika uchaguzi mkuu wa urais.

Akiwahusia Wamarekani wasiogope ugonjwa wa corona katika ujumbe wake wa awali kwenye Twitter siku ya Jumatatu, Bw. Trump aliongezea kusema: "Utawala wa Trump, umetengeza dawa na kujifunza mengi. Najihisi vyema zaidi kuliko miaka 20 iliyopita!!"

Latest News

ETHIOPIA YASEMA HAITISHWI NA TAMKO LA RAIS DONALD TRUMP.
24 Oct 2020 16:54 - Grace Melleor

Waziri mkuu wa Ethiopia amesema nchi yake "haitakubali vitisho vya aina yoyote" baada ya Rais Donald Trump kusema kuwa M [ ... ]

RAIS TSHISEKEDI ATANGAZA MASHAURIANO YA UMOJA KWA MUUNGANO TAWALA.
24 Oct 2020 06:41 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi, katika hotuba yake kwa taifa aliyoitoa siku ya Ijumaa wiki hi [ ... ]

SEKTA YA AFYA NCHINI YAPATA NEEMA KUTOKA USWISI.
23 Oct 2020 15:23 - Grace Melleor

Serikali imepokea msaada wa Faranga za Uswisi Milioni 15.75 sawa na shilingi Bilioni 39.59 kwa ajili ya kugharamia mradi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.