Star Tv
Picha ya kusisimua ya sokwe na mmoja wa waokoaji wake imeshinda tuzo la mpigapicha bora wa mwaka la Chaguo la Watu au 'People's Choice'.Picha hii iliyoshinda tuzo la mwaka ilichukuliwa na mpigapicha wa Canada, Jo-Anne McArthur ilionesha sokwe huyo mdogo, kutoka eneo la nyika Tambarale ambaye aliokolewa na kampuni ya Ape Action Africa kutoka kwa wawindaji haramu. Katika picha hii anaonekana kwenye mikono ya mchungaji wake, Appolinaire Ndohoudou, wakati alipokuwa akisafirishwa kutoka kwenye makazi madogo ya sokwe hadi kwenye makao salama ya msitu wa Cameroon, ambako kuna msitu mpana zaidi. "'Ninashukuru sana kwamba picha hii imewagusa watu na ninatumai inaweza kutufundisha sote kuwajali walau kidogo wanyama," anasema McArthur. "Hakuna kitendo chochote cha ukarimu kwao kinachokua kidogo sana" "'Mara kwa mara ninarekodi ukatili wanaopitia wanyama katika mikono yetu, lakini wakati mwingine ninashuhudia taarifa za uokozi, matumaini na ukombozi wao." Picha hii ilichaguliwa takriban mara 20,000 na mashabiki wa mazingira kutoka kwenye orodha ya picha 24 zilizochaguliwa na makavazi ya kihistoria ya mali asili, ambazo zilichaguliwa kati ya picha from takriban 50,000 zilizowashilishwa kwa ajili ya shindano la kuwania tuzo la picha bora ya mwaka 2017. Add a comment
Mwanamume aliyejibadilisha jinsia na kuwa mwanamke amefanikiwa kumyonyesha mtoto katika kisa cha kwanza cha iana yake kuwahi kushuhudiwa, watafiti wanasema. Mwanmke huyo mwenye umri wa miaka 30 alitaka kumnyonyesha mtoto baada ya mpenzi wake aliyejifungua kusema hataki kumnyonyesha mtoto huyo, hayoni kwa mujibu wa wa jarida la afya la watu waliojibadili jinsia. Alifanikiwa kunyonyesha baada ya kumeza dawa na kukamua maziwa, ripotihiyo inasema kutoka nchini Marekani. Mtaalamu wa Marekani anasema utafiti huo huenda ukachangia visa zaidi vya wanaume walijibadilisha jinsia kuwa wanawake kunyonyesha watoto. Mwanamke huyo aliyekuwa anapokea matibabu ya kubadili homoni zake mwilini kwa muda wa miaka 6, lakini hajafanyiwa upasuaji kubadili sehemu zake za siri, wakati alipowaomba madaktari wamsaidie atimize lengo lake la kumnyonyesha mtoto. Kabla ya mtoto huyo kuzaliwa, madakatari walimpadawa za miezi mitatu unusu kumsaidia kupata maziwa, kwa kawaida dawa hizo hupewa wanawake waliowaasili watoto au waliojipatia watoto kupitia wanawake wanobeba mimba kibiashara kuwaisaidia wasioweza kuzaa. Dawa hizo husisimua homoni mwilini kushinikiza kutoa maziwa na kuzuia homoni za kiume na pia alihitajika kukamua maziwa yake. Na mtokeo yake, yalimsababisha mwanamke huyo kuweza kupata maziwa kiasi. Watafiti wanasema mtoto huyo alikunywa maziwa hayo tuu kwa wiki zake sita za uhai, wakatiambapo ukuwaji wake, ulaji na uwendaji haja wake ulikuwa unaendelea kama kawaida. Baada ya hapa, mtoto alianza kupewa maziwa ya mkebe kwasababu maziwa yalianza kupungua. Mtoto huyo sasa ana miezi sita na anendelea kunyonya kama sehemu ya lishe yake, wahiriri wa utafiti huo wanasema. Add a comment
Mwanamke mmoja wa China aliandamana na begi lake kupitia mashine ya ukaguzi ya X -Ray. Wafanyikazi katika kituo cha reli cha Kusini mwa China walishangazwa kuona mwanamke huyo akitoka ndani ya mashine hiyo pamoja na begi lake. Video moja ya mtandaoni ilionyesha kisa hicho cha kushanganza kilifanyika siku ya Jumapili baada ya kuupanda ukanda wa kusukuma mizigo. Awali mwanamke huyo alitazama begi lake likiwekwa katika mshipi huo na kuondoka.Picha za mionzi ya X-Ray zilimuonyesha mwanamke huyo akiwa amepiga magoti nyuma ya begi lake huku akiwa amevaa viatu virefu. Haijabainika ni kwa nini mwanamke huyo hakutaka kuwa mbali na begi lake ,lakini raia wengi nchini China hubeba kiwango kikubwa cha fedha wakati wanapoelekea nyumbani kusherehekea mwaka mpya. Add a comment
Maafisa wa polisi nchini India wamemkatama mwanamke mmoja aliyejifanya kuwa mwanamume na kuwadanganya wanawake wawili ili kulipwa mahari. Krishna Sen alikamatwa siku ya Jumatano katika jimbo la Kaskazini la Uttarakhand kwa kutaka kulipwa mahari kinyume na sheria nchini India. Maafisa wa polisi waliambia BBC kwamba iligunduliwa wakati wa mahojiano kwamba Krishna alikuwa mwanamke. Wanaamini bi Sen mwenye umri wa miaka 26 aliyejulikana kama 'sweety' amekuwa akijidai kuwa mwanamume tangu 2014 wakati alipooa kwa mara ya kwanza.Bi Sen inadaiwa aliachana na mke wake wa kwanza mara tu baada ya harusi na mke wake wa kwanza na kumuoa mwanamke mwengine mnamo mwezi Aprili 2017. Lakini mashemegi zake waliwasilisha malalamishi wakimshutumu kwa kumnyanyasa mwanao ili kulipwa mahari. Pia walidai kwamba alikuwa amewaomba takriban dola 13,297 ili kuanza biashara na kwamba hakurudisha fedha hizo. Kulipa na kukubali mahari ni utamaduni wa karne moja iliopita Kusini mwa India ambapo wazazi wa mke hulipa fedha, nguo na vito kwa familia ya mume. Ijapokuwa utamaduni huo ni kinyume na sheria nchini India tangu 1961, unaendelea. Maafisa wa polisi walisema kuwa bi Sen aliwaambia kwamba amekuwa akitaka kuwa mvulana na kuishi kama mume akiongozea haijulikani iwapo wazazi wa bi Sen walikuwa wanajua kile ambacho amekuwa akifanya. Wanawake wote aliowaoa hawakumshuku. Bi Sen hakuvua nguo mbele yao na kulingana na polisi hakushiriki nao katika tendo la ngono. Alikuwa na marafiki wa kiume, akitumia vyoo vya wanaume na kuzungumza kwa kutumia sauti tofauti , polisi wanasema. Pia alidaiwa kuvuta sigara, kunywa pombe na kuendesha pikipiki na marafikize wa kiume, ili kuondoa shauku yoyote. Akiwa amenyolewa kama mwanamume, kuvaa na kuwa na tabia za kiume Krishna alikuwa akiishi maisha ya kiume. Hakuna mtu aliyemshuku Krishina, afisa mwengine wa polisi alisema. Add a comment
Mamlaka nchini Peru zimemkamata mfungwa zaidi ya mwaka mmoja tangu atoroke jela kwa kumuacha ndugu yake pacha katika nafasi yake Alexander Delgado alikuwa akitumikia kifungo cha miaka 16 wa dhuluma ya kingono kwa mtoto na wizi kwenye gereza moja kaskazini mwa Lima. Wakati ndugu yake pacha alimtembela gerezani mwezi Januari mwaka uliopita, Alexander alimwekea dawa ya kulevya, akambadilisha nguo zake na kutoroka jela. Mabadiliko hayo kwa wafungwa yalithibitiswa wakati alama za vidole za Giancarlo zilichukuliwa.Baada ya miezi 13 mafichoni Alexander Delgado alaikamatwa siku ya Jumatatu katika mji wa bandari wa Callao baada ya wizara ya masuala ya ndani kutangaza zwadi kuhusu bahari ambazo zingepelekea akamatwe. Sasa anatarajiwa kuhamishwa kwenda kwa grereza lenye ulinzi mkali kusini mwa nchi. Wakati Alexander akiwa mafichoni ndugu yake Giancarlo alikamatwa na kuchunguzwa akishukiwa kushirikiana na pacha wake. Lakini hakushtakiwa na sasa ameachiliwa. Akiongea na vyombo vya habari Alaxander Delgadoi alisema alitotoroka kwa sababu alikuwa ana hamu sana ya kumuona mama yake. Add a comment

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.