Star Tv

Balozi wa China nchini Marekani anasema kuwa China haitatuma silaha na risasi kusaidia vita vya Urusi nchini Ukraine na kwamba Beijing "itafanya kila kitu ili kupunguza mzozo".

Maoni ya Qin Gang yanakuja baada ya Rais wa Marekani Joe Biden kumuonya mwenzake wa China Xi Jinping siku ya Ijumaa kwamba kutakuwa na "matokeo" ikiwa Beijing itatoa msaada wa kijeshi kwa Moscow.

Beijing ilikanusha ripoti za wiki jana kwamba ilikuwa tayari kuipatia Moscow silaha kama "habari zisizofaa", lakini Uchina imekuwa ikisita kuikemea Urusi kwa uvamizi wake.

Akizungumza na shirika la utangazaji la Marekani CBS, Gang alilalamika kwamba kulaaniwa na nchi za Magharibi "hakusaidii" na kwamba "diplomasia nzuri" inahitajika.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.